Nenda kwa yaliyomo

Party of National Unity (Kenya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka PNU)

Party of National Unity (kifupi: PNU; pia: Chama cha Umoja wa Kitaifa) ni muungano wa vyama vya kisiasa nchini Kenya ulioanzishwa tarehe 16 Septemba 2007 kabla ya uchaguzi mkuu wa rais na bunge. Kusudi lake lilikuwa kuunganisha vikundi vyote vilivyosimama upande wa rais Mwai Kibaki aliyejiandaa kugombea urais mara ya pili dhidi ya upinzani wa Orange Democratic Movement (ODM).

Rais Mwai Kibaki wa Kenya alitangaza muungano huo mpya na akasema kuwa angeweza kugombea kiti cha urais na chama hicho katika uchaguzi wa Kenya wa Desemba 2007 lakini tangu kimekuwa chama cha kisiasa katika haki yake yenyewe, kufuatia masharti yaliyowekwa na kielezo cha Vyama vya Siasa kilichopitishwa Kenya mwaka 2008.

Muhtasari

[hariri | hariri chanzo]

PNU ilianzia kama muungano wa vyama kadhaa, vikiwemo: KANU, NARC-Kenya, Ford-Kenya, FORD-People, Democratic Party, Shirikisho na vingine. Rais Mwai Kibaki tu ndiye angekuwa mhusika binafsi wa PNU kando ya ushiriki wa vyama vyote husika.

PNU iliundwa muda mfupi kabla ya uchaguzi wa mwezi Desemba 2007. Hadi mwanzo wa Septemba haikuwa wazi ni tiketi ya chama gani rais angetumia katika uchaguzi. Katika uchaguzi wa mwaka 2002, Kibaki alikuwa mgombea wa National Rainbow Coalition (NARC), ambayo ilikuwa tangu imetengana. NARC ya hapo awali ilikuwa kisheria katika mikono ya Charity Ngilu ambaye hakutaka kujiunga na kibaki kwa jitihada jipya. Washirika wa kibaki walikuwa wameshajitoa NARC na kuunda NARC-Kenya ambayo haikuwafurahisha wanasiasa kadhaa wa muhimu katika Serikali ya Muungano ya Kibaki ambayo ilikuwa imewachukuwa wanasiasa waliokuwa wa upinzani hapo awali na bado walivishikilia vyama vyao kama KANU au Ford-Kenya..[1]

Vyama shiriki katika PNU

[hariri | hariri chanzo]

Vyama vifuatavyo vilitangazwa kuwa vimeunga mkono katika PNU [1] Ilihifadhiwa 2 Januari 2008 kwenye Wayback Machine.:

Vyama vingine ambavyo havikutajwa kwenye tovuti rasmi vilishiriki pia kama, kwa mfano, Ford-Asili, FORD-People na vingine vidogo.

Wakati ilianzishwa, mwaka 2007, chama kilikuwa na Mwai Kibaki kama mwanachama wa kibinafsi, na vyama vyote vingine husika vilijiunga kama shirika binafsi. Hata hivyo, katikati ya 2008 chama hiki kilianza kuwa na uchaguzi ndogo ndogo ili waweze kuwa na miungo halisi ili iwe chama katika haki yake yenyewe. Ingawa majaribio ya kufanya vyama-husika vijiunge na PNU yalishindwa.

muundo wa uongozi wa chama una ya kiongozi wa chama, Mwenyekiti wa Taifa, Katibu Mkuu, na Wenyeviti wa Mikoa.[2][3]

Maandalizi ya chama kipya

[hariri | hariri chanzo]

PNU iliundwa haraka inaonekana bila maandalizi mazuri. Hadi mwanzo wa Septemba 2007 haikueleweka Kibaki atagombea urais kupitia chama gani. Chama cha NARC kilichokuwa chombo cha Kibaki mwaka 2002 ilikuwa mkononi mwa mwenyekiti wake Charity Ngilu asiyeonyesha dalili la kumwunga Kibako mkono. Wanasiasa wengi wa upande wa Kibaki waliwahi kuacha NARC na kujenga badala yake NARC-Kenya lakini kikundi hiki hakikujenga uhusiano mzuri na wanasiasa wa serikali ya umoja wa kitaifa walionekana kuwa muhimu kwa Kibaki kama vile Simon Nyachae wa FORD-Kenya au Njenga Karume wa KANU.[4]

Mapatano ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Hivyo PNU iliundwa katika muda mfupi. Mipango ya awali ilikuwa kumpigania Kibaki kama rais na kuwa na wagombea wa pamoja kwa bunge na ngazi ya miji na tarafa. KANU ilikubaliwa kuwa na wagombea wake wa pekee kwa ajili ya bunge.

Ukosefu wa umoja

[hariri | hariri chanzo]

Lakini baadaye vyama vingine vilisisitiza pia kuwa na wabunge wao kwa jina la chama. Kwa hiyo FORD-Kenya, Mazingira, Sisi kwa Sisi na NARC-Kenya vilipeleka wagombea wao mahali pengi pamoja na wagombe katika jina la PNU. Kwa hiyo palikuwa na mashindano mahali mbalimbali kati ya vyama vilivyokubaliana kuwa PNU.

Uchaguzi Mkuu wa 2007

[hariri | hariri chanzo]

Maandalizi duni ya chama hiki yalijitokeza katika harakati za uteuzi wa viti vya bunge. Awali, wanachama wa PNU walikubali wagombea wa viti vya bunge wajisajili chini ya PNU, isipokuwa KANU, ambayo iliruhusiwa kusajili wanachama wake pekee.[5] Hata hivyo, mkataba huu haukusonga mbele. Kama matokeo, baadhi ya wagombea-hasa kutoka chama cha Kibaki cha awali cha Democratic Party-walitumia tiketi ya PNU na wengine walitumia tiketi za vyama husika. Katika majimbo kadhaa wanachama-husika wa PNU walijipata wakigombea kiti kimoja.

Matokeo ya uchaguzi 2007

[hariri | hariri chanzo]

Kwa jumla PNU haikufaulu kupata viti vingi bungeni kadiri ya matokeo yaliyopatikana hadi 3 Januari 2008. Vilukuwa 43 kati ya 210 kulingana na 99 vya wapinzani wao wakuu, ODM na 15 kwa ODM-K. Viongozi wengi hasa mawaziri wa serikali ya umoja wa kitaifa walishindwa kushika viti bungeni.

Pamoja na vyama vingine vilivyoungana mkono kumpigania Kibaki idadi iliweza kufikia wabunge kama 78.

Tarehe 28 Februari 2008 kupitia timu ya upatanishi iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, serikali ya PNU ilifikia mkataba na ODM ya Raila Odinga kugawana madaraka. Mpango wa kugawana madaraka ulikuwa wa kwanza wa aina yake barani Afrika.

Tangu mwaka 2008

[hariri | hariri chanzo]

Tangu uchaguzi wa 2007, PNU imejiandikisha kama chama halisi cha kisiasa ikiwa na George Saitoti kama mwenyekiti na Mwai Kibaki kama kiongozi wa chama, kitu kilichowafadhaisha wanachama wengi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]