ODM-Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wiper Democratic Movement ni chama cha kisiasa nchini Kenya. Chama kilianzshwa mwaka 2006 katika maandalizi ya uchaguzi wa bunge la Kenya 2007 ikijulikana kama Orange Democratic Movement-Kenya. Katika Agosti 2007 chama kilifarakana kati ya wafuasi wa Kalonzo Musyoka aliyeendelea kwa ODM-Kenya na maungano ya viongozi wengi zaidi pamoja na Raila Odinga walioendelea kama Orange Democratic Movement. Sababu ya farakano ilikuwa swali la nani atakuwa mgombea wa urais upande wa ODM.

Chanzo cha ODM katika kura ya katiba mpya[hariri | hariri chanzo]

Chanzo cha ODM ilikuwa kura maalumu ya wananchi ya 2005 kuhusu katiba mypa. Katiba ilipendekezwa na rais Mwai Kibaki na wafuasi wake. Wabunge wa LDP walipinga pendekezo la katiba pamoja na chama cha upinzani cha KANU chini ya Uhuru Kenyatta. Pande mbili katika kura hii zilipewa alama za ndizi (kambi ya "ndiyo") na chungwa (kambi ya "hapana"). LDP na KANU zilishirikiana pamoja katika kambi ya machungwa. Baada ya katiba kukataliwa na wananchi katika kura maalumu Kibaki aliondoa wafuasi waote wa kambi la machungwa katika serikali yake.

Kuunda chama na farakano[hariri | hariri chanzo]

Hapa waliamua kuandaa chama kipya pamoja na KANU kwa ajili ya uchaguzi wa 2007. KANU ilijiondoa kabla ya uchaguzi lakini viongozi kadhaa kama vile Musalia Mudavadi na William Ruto walibaki upande wa ODM. Swali la kumteua mgombea wa urais iligawa ODM kwa sababu viongozi mbalimbali walitaka kushika nafasi hii. Hii ilileta farakano kati ya ODM chini ya Raila Odinga na ODM-Kenya chini ya Kalonzo Musyoka.

Uchaguzi wa 2007[hariri | hariri chanzo]

Katika uchaguzi wa 2007 ODM-Kenya haikutokea kama chama cha kitaifa. Kilikuwa na nguvu katika Ukambani ilipochukua majimbo ya uchaguzi 13 kati ya 17 za Ukambani. Ikaongeza majimbo mawili ya Bura na Saku nje ya Ukambani, jumla la wabunge 15.[1] Kalonzo Musyoka alipata asilimia 9.5 za kura katika uchaguzi wa rais akamaliza nafasi ya tatu. Alitangaza atakuwa tayari kuingia katika ushirikiano na rais atakayechaguliwa. Baada ya uchaguzi ODM-K iliingia katika serikali ya mseto na PNU ya Mwai Kibaki. Kiongozi wake Musyoka alipewa nafasi ya makamu wa rais na mwenyekiti wa chama Samuel Poghisio akawa waziri wa mawasiliano na habari kati ya mawaziri 15 wa kwanza walioteuliwa na Kibaki baada ya uchaguzi wake uliopingwa na ODM.

  1. Voters defy ODM-K ‘wiper’ wave eastandard 30-12-2007 - imeangaliwa 5-01-2008

. Mwaka 2011 jina ya chama hiki ilibadilishwa kuwa Wiper Democratic Movement, ili kuwezesha wafuasi wake kuitofautisha na chama cha ODM. [1]

  1. http://www.standardmedia.co.ke/InsidePage.php?id=2000042124&cid=4