Ruth Bosibori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ruth Bosibori

Ruth Bosibori Nyangau (pia huandikwa kama Ruth Bisibori, alizaliwa 2 Januari 1988 huko Bosiango) ni mwanariadha Mkenya anayekimbia katika mashindano ya umbali wa kati na ni mtaalamu katika shindano la steeplechase mita 3,000.

Mwezi Julai 2007 alikuwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya All-Africa Games, kwani ilishindaniwa mara ya kwanza mwaka huo. Mwezi Agosti mwaka uo huo alimaliza wa nne katika Mashindano ya dunia katika rekodi ya dunia ya wanariadha wachanga yadakika 9:25.25. Rekodi ya awali ilikuwa 9:30.70 ilikuwa imewekwa na Melissa Rollison. [1]. Alimaliza wa tatu katika mashindano ya Mabingwa wa Afrika mwaka 2008.

Bosibori alizaliwa katika kijiji cha Bosiango kilicho karibu na Kisii [2] Alianza kukimbia mwaka 2003 alipokuwa katika chuo cha upili cha Kebirichi. Aliajiriwa na Polisi wa Kenya baada ya kushinda michuano ya mkoa mwaka 2007 [3] Amezoea kukimbia mguu tupu.[4]

Alishinda tuzo la Mwanariadha wa kike ambaye ana ahadi zaidi mwaka 2007 katika sherehe za Kenya Sports Personality of the Year[5] Kocha wake ni Dan Muchoki [6]

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

mwaka Mchuano Ukumbi Tokeo Ziada
2007 All-Africa Games Alger, Algeria 1 3000 m steeple
World Championships Osaka, Japan 4 3000 m steeple
2008 African Championships Addis Ababa, Ethiopia 3 3000 m steeple
Michezo ya Olimpiki Beijing, Uchina 6 3000 m steeple
World Athletics Final Stuttgart, Ujerumani 3 3000 m steeple
2009 World Championships Berlin, Ujerumani 7 3000 m steeple
World Athletics Final Thessaloniki, Grekland 1 3000 m s'chase

Marejeo[hariri | hariri chanzo]