2 Januari
Mandhari
| Des - Januari - Feb | ||||||
| 1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
| 8 | 9 | 10 | 11 | 12 | 13 | 14 |
| 15 | 16 | 17 | 18 | 19 | 20 | 21 |
| 22 | 23 | 24 | 25 | 26 | 27 | 28 |
| 29 | 30 | 31 | ||||
| Kalenda ya Gregori | ||||||
Tarehe 2 Januari ni siku ya pili ya mwaka. Mpaka uishe zinabaki siku 363 (364 katika miaka mirefu).
Matukio
[hariri | hariri chanzo]| Mwaka | Tukio |
|---|---|
| 1492 | Mfalme Boabdil wa Granada anasalimisha mji wake kwa wafalme wa Hispania – mwisho wa utawala wa Kiislamu katika rasi ya Hispania |
| 1956 | Nchi ya Sudani inapata uhuru kutoka Misri na Uingereza |
| 1984 | Nchi ya Brunei inapata uhuru kutoka Uingereza |
| 1993 | Nchi ya Chekoslovakia inagawanywa kuwa nchi huru mbili, Ucheki na Slovakia |
Waliozaliwa
[hariri | hariri chanzo]| Mwaka | Tukio |
|---|---|
| 869 | Yozei, mfalme mkuu wa Japani (884–887) |
| 1837 | Mily Balakirev, mtunzi wa muziki kutoka Urusi |
| 1909 | Shaaban Robert, mshairi wa Kiswahili kutoka Tanzania |
| 1909 | Barry Goldwater, mwanasiasa kutoka Marekani |
| 1911 | Audrey Wurdemann, mshairi kutoka Marekani |
| 1941 | Martin Evans, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba mwaka wa 2007 |
| 1941 | Evaristo Marc Chengula, askofu wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Tanzania |
| 1950 | Mudhihir Mohamed Mudhihir, mwanasiasa wa Tanzania |
| 1953 | Alpha Blondy, mwanamuziki kutoka Côte d'Ivoire |
| 1954 | Sigfrid Selemani Ng'itu, mwanasiasa wa Tanzania |
| 1960 | Julius Nyaisangah, mtangazaji wa redio kutoka Tanzania |
| 1962 | Richard Roxburgh, mwigizaji wa filamu kutoka Australia |
| 1967 | Tia Carrere, mwigizaji wa filamu kutoka Hawaii |
| 1988 | Ruth Bosibori, mwanariadha kutoka Kenya |
| 1992 | Jack Wilshere, mchezaji mpira kutoka Uingereza |
Waliofariki
[hariri | hariri chanzo]| Mwaka | Tukio |
|---|---|
| 379 | Mtakatifu Basil wa Caesarea, askofu na mwalimu wa Kanisa kutoka Uturuki |
| 457 | Markian, Kaizari wa Dola la Roma Mashariki (450–457) |
| 1833 | Mtakatifu Serafino wa Sarov, mmonaki padri kutoka Urusi |
| 1954 | Leonard Bacon, mshairi kutoka Marekani |
| 1995 | Eugene Wigner, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1963 |
| 2008 | Lucas Sang, mwanariadha wa Kenya |
Sikukuu
[hariri | hariri chanzo]- Wakristo wengi, wakifuata mapokeo ya Roma, huadhimisha kumbukumbu ya watakatifu Basili Mkuu na Gregori wa Nazienzi, lakini pia za watakatifu Papa Telesforo, Arjeo, Narsisi na Marselino, Teodoro wa Marseille, Bladolfo, Yohane Bono, Visensiani, Mainchin, Adalardo wa Corbie, Airaldo, Silvesta wa Troina n.k.
- Waorthodoksi wanaadhimisha sikukuu ya mtakatifu Serafino wa Sarov
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu 2 Januari kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
