Nenda kwa yaliyomo

Msitu wa Kakamega

Majiranukta: 0°17′30″N 34°51′22″E / 0.29167°N 34.85611°E / 0.29167; 34.85611
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Msitu Kakamega)
Msitu wa Kakamega.

Msitu wa Kakamega uko katika Kaunti ya Kakamega na Kaunti ya Nandi, Kenya, kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi, na karibu na mpaka na Uganda. Inasemekana kuwa mojawapo wa mabaki ya mwisho ya Kenya ya msitu wa mvua wa kale wa Guineo-Congolian uliozingira wakati mmoja bara la Afrika.

Ikiwa ni pamoja na hifadhi ya wanyamapori, misitu huu umezingira takribani kilomita za mraba 230, ambapo ni chini ya nusu ambayo kwa sasa inabakia kama misitu ya asili. Kuna maeneo mengi nyasi ilikokatwa na maeneo yaliyo bure Utajiri wa msitu huu kwa aina tofauti za ndege, wadudu na wanyama wa aina ya reptiles huifanya kuwa kivutio kikuu cha watalii wanaopenda kutazama ndege wapiga picha za wanyamapori. Hakuna shughuli kuu za kiutalii na Msitu Kakamega siyo kivutio kikuu cha watalii. Wanyama wakubwa ni nadra. Sehemu ya msitu pia ina makazi ya wanyama ya kipekee ya aina ya nyanda za juu, lakini kwa ujumla, mimea na wanyama kwenye Msitu huu hazichapta kuchambuliwa kwa upana na sayansi. Hali ya hewa ni ya mvua sana kukiweko za zaidi ya mita mbili za mvua kwa mwaka. Misimu za mvua ni Aprili hadi Mei na Agosti hadi Septemba.

Kaskazini ya Msitu huu ni Hifadhi ya Kitaifa ya Kakamega, iliyopewa sifa ya kuwa hifadhi ya Kitaifa mwaka wa 1985. Kaskazini kwake ni Msitu wa Hifadhi wa Kisere. Licha ya kuwa misitu wa hifadhi, msitu huu umeendelea kuharibiwa sana. Idara ya Misitu ya Kenya na Shirika la Kenya la Wanyamapori zinafanya kazi ili kulinda msitu huu. Wakaazi wa eneo hili ni Waluhya, ambao wanategemea msitu huu kwa mahitaji yao yote. Kanda hii inasemekana kuwa mojawapo ya maeneo yenye watu wengi zaidi vijijini ulimwenguni, na shinikizo kwenye rasilimali ya msitu huu ni kubwa. Mradi unaofadhiliwa na Ujerumani wa BIOTA East umekuwa ukifanya kazi katika msitu huu tangu mwaka wa 2001, ambapo kwanza, rekodi ya kila aina ya maisha kwenye msitu huu ilifanywa na la lengo kupanga mikakati ya matumizi endelevu ya msitu huu mpaka mwaka wa 2010.

Barabara kuu ya A1 inapita magharibi ya eneo hili.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

0°17′30″N 34°51′22″E / 0.29167°N 34.85611°E / 0.29167; 34.85611