Nenda kwa yaliyomo

Sakawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sakawa alikuwa nabii wa kale wa Abagusii aliyetabiri kuja kwa Mtu mweupe au Mzungu. Aliwaonya Wakisii kuwa watawanyag'anya vitu vyao kama mashamba, ng'ombe na mavuno yao.

Kuzaliwa

[hariri | hariri chanzo]

Inasemekana alizaliwa miaka 1838-1840 Kisii kusini. Alikuwa mtu aliyependa kunyamaza sana, lakini hawakujua kunyamaza kwake ndiko kulimfanya kuwa na busara na hekima.

Aliheshimika sana na pia alikuwa na nguvu za kutabiri kitu na kufanyika.

Kukumbukwa

[hariri | hariri chanzo]

Atakumbukwa kwa vile kuna wakati janga liliwadia kwa Wakipsigis, janga la kuua wanyama, lakini Sakawa aliombea hilo janga na halikumuua mnyama yeyote wa Wakisii. Wakipsigis walihisi wivu na wakataka kuwavamia Wakisii. Sakawa aliambiwa afanye jambo. Sakawa alituma ndege wengi waliowavamia Wakipsigis. Lakini hawakuvunjika moyo waliwavamia wakisii na kuwanyanganya mifugo yao.Sakawa aliwabariki vijana walioenda kufuata mifugo yao ,walisikia sauti ya mifugo yao huko Manga na waliwachukua mifugo yao.

Inasemekana alitabiri kifo chake. Alikufa kwa kiti chake cha miguu mitatu cha kale. Kuna mti unaoheshimika sana na Wakisii ambao unaitwa sakawa unaodhaniwa ndipo alipozikwa. Inasemekana tena alipotelea hakuonekana.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sakawa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.