Waluo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wajaluo)
Jump to navigation Jump to search

Waluo (pia Wajaluo) ni kabila hasa la Sudan Kusini. Wako pia Kenya, Uganda na mashariki mwa Tanzania katika Mikoa ya Mara na Mwanza. Lugha yao ni Kiluo. Wenyewe hujiita Jaluo na lugha yao Dhulou.

Waluo ni mkusanyiko wa kabila la Kiniloti ambalo lilisafiri kutoka Afrika ya Kaskazini kufuata mto Nile kuja Kusini. Waluo wengi wameenea kandokando ya Ziwa Viktoria kutokana na utamaduni wao wa uvuvi.

Wajaluo mashuhuri

  • Philemon Sarungi - Mtaalam wa udaktari na kiongozi nchini Tanzania
  • Gidi Gidi Maji Maji - Wasanii wa muziki aina ya hip hop
  • Tom Mboya - mwanasiasa aliyeuawa 1969
  • Barack Obama - mwanasiasa na Rais wa Marekani ni mwana wa baba Mjaluo
  • Jaramogi Oginga Odinga - mwongozi wa Wajaluo kutoka wakati wa kupigania uhuru, mwanzilishaji wa vyama vya KANU, KPU, FORD-Kenya na makamu wa rais wa kwanza
  • Raila Amolo Odinga - mwana wa Jaramogi na mwanasiasa muhimu wa kitaifa
  • Robert Ouko - hayati waziri wa mambo ya kigeni aliyeuawa 1990.(Hayati Daniel owino missiani mwanamuziki mtanzania aliyewahi kuwania tuzo la muziki aina ya rhumba huko nchini kenya alifariki mwaka 2006 nakuzikwa huko shirati rorya.wajaluo wengine maarufu ni Riaga ogalo.ni mwenyekiti wa wajaluo afrika mashariki,baadhi ya wazee maarufu wilayani rorya ni kama,mtemi odemba kagose wa buturi.mtemi ochuodho awino wa kamageta. pia mzee mirimbo oreck ragare huyu ndiye mzee wa kwanza kamageta kununua baiskeli, alikufa mwaka 1999 huko kamageta ktk kijiji cha osiri.daniel opanga oole wa kamageta(babake balozi joshua watson opanga) alifariki mwaka 1992 ndiye mwanzilishi wa kanisa la menonite huko kamageta kata ya roche rorya,wengine ni timothy apiyo waziri mkuu mstaafu wa watanzania.

Viungo vya nje

  • [www.jaluo.com]
Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waluo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.