Wamambwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wamambwe ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Rukwa, Wilaya ya Sumbawanga. Wako pia upande wa Zambia. Lugha yao ni Kimambwe. Wamambwe na Warungu wanaongea lugha moja yenye lahaja mbili.

Ni wakulima wa maharage, mahindi, ulezi mhogo, viazi na mboga za majani. Ukisikia wanaongea utafikiri Kifipa lakini maneno yao mengi wanapenda kuchangaya na kiingereza.

Asili ya kabila la Wamambwe ni Zambia hasa eneo karibu na mji wa Mbala. Wanapenda kula ugali na mahrage na mlenda uitwao mpondesha yaani mlenda mzito. Vile kamaa jamii nyingine za kibantu ni wafugaji na wawindaji wadogo.

Koo zao kwa upande wa wanaume mara nyingi huanzia na "Si" mfano Sinyagwe, Sichula, Siame, Sikonda, Simfukwe, Sichone, Simuyemba, Simpokolwe, Simte, Sikaumbwe, Simchile, Simpanzye, Sikalumba.

Kwa upande wa wanawake huanzia kwa "Na" mfano Nanyangwe, Nachula, Namfukwe, Nayame, Nakonda, Nachone, Namuyemba, Nampokolwe, Namte, Nakaumbwe, Nnampanzye, Nakalumba n.k. Wakati Wafipa asili hawana majina hayo ila wenyewe utasikia Nandi, Kapufi, Kipesha, Chula, Ngua, Nyami na mengineyo.

Halafu tabia yao mtoto mdogo anapomwita mtu mkubwa kuonyesha heshima lazima amwite kwa uwingi yaani mtu mmoja anaitwa kama watu wengi mfano baba kwa Kimambwe huitwa tata kiheshima ataitwa YATATA mama huitwa mayo kiheshima YAMAYO.

Ni kabila ambalo kwa kuongea wanafanana na Walungu utofauti wao upo kwa mambo madogo madogo kama vile ngoma za asili, adabu ,usafi, ukali na haraka ya kuongea. Asili ya mambwe ni upole wakati mlungu hataki mchezo ila mmambwe akichukia anachukia kikweli kweli.

Ukoo mkubwa wa kichifu kwa upande wa Wamambwe ni akina Sichula kama vile Kutazungwa,Mfwambo,Mwamba Sokoro n.k. wakati kwa Walungu ni akina Sikazwe na Sichilima kama vile Tafuna, Kapembwa,Zombe, Londe n.k.

Vile Wamambwe ni wafanya biashara ya mazao ya mahindi na maharage. Ukiangalia kwa upande wa wamabwe walioko Zambia wamepiga hatua kutokana na miundo mbinu waliojengewa na taifa lao ndio hata wale waliosoma sana wanapatikana ile nchi. Tatizo linalosumbua kwa upande wa Tanzania ni miundo mbinu mibovu kiasi kwamba jamii hii iaonekana kama haipo Tanzania ndio maana watu wengi huona kama kabila geni nchini.


Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamambwe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Wamambwe" ni fupi mno. Inahitaji kupanuliwa mapema.