Wakara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wakara ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Mwanza, katika wilaya ya Ukerewe, Kisiwani UKARA. Lugha yao ni Kikara.

Wakara ni kabila linalopatikana katika nchi ya Tanzania. Wakara wanaishi Mkoani Mwanza, Wilaya ya Ukerewe katika kisiwa cha Ukara. Kutokana na uhaba wa ardhi uliotokana na ongezeko la kasi la idadi ya watu, Wakara wengine wamelazimika kuhama kutoka kisiwa hicho. Kwa sasa wanapatikana kwa wingi katika kisiwa cha Ukerewe, wilaya za Sengerema, mkoani Mwanza, Geita mkoani Geita na Chato mkoani Kagera. Lugha yao ni Kikara. Lugha yao inafanana sana na Kijita na Kikwaya, lugha ambazo huzungumzwa na Wajita na Wakwaya; makabila ambayo hupatikana mkoa wa Mara. Hata majina yao hufanana. Haya makabila yana mila ambazo vilevile zinafanana sana.

Hata hivyo ipo tofauti ndogondogo sana katika matamshi ya lugha hizi. Kwa mfano, badala ya maneno yenye "g" kutamkwa na Wakara, wao hutamka "k" tofauti na wenzao Wajita na Wakwaya. Pia kuna maneno yenye herufi "J". Wakati Wajita na Wakwaya hutamka maneno yenye "J" kama yalivyo, wenzetu Wakara hutamka maneno hayo kama "ch".

Mifano halisi ni kama ifuatavyo:-

Wajita Wakara Chigende (twende) Chikende Jaji (babu) Chachi Magesa (Jina la mtu) Makesa Inasemekana kuwa asili ya wakara ni kutoka Sudani ya Kusini. Inaaminika Wakara walikimbia vita ya kusaka biashara ya watumwa, wakipitia Uganda na hatimaye kujikuta katika kisiwa cha Ukara ambapo waliamua kuweka maskani. Kundi hili hupatikana zaidi katika sehemu ya magharibi ya kisiwa hiki. Hata hivyo kuna jamii ya watu wachache ambao walitokea sehemu ya mashariki katika mkoa wa Mara.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.