Mboga


Mboga ni sehemu za mimea zinazopikwa na kuliwa kama chakula cha kibinadamu. Kwa kawaida tunda, jozi, mbegu au nafaka hazihesabiwi kati ya mboga.
Mifano ya mboga ni:
- mboga majani kama sukumawiki, spinachi, kabeji, mchicha, chainizi, mgagani, mnavu, matembele,kisamvu, majaniyaboga na majaniyakunde
- shina kama kitunguu, liki n.k.
- mizizi kama karoti, figili n.k.
- matunda kama nyanya, pilipili n.k.
Chakula cha mboga chaingiza vitamini na madini muhimu katika mwili.
Chakula cha kupikwa[hariri | hariri chanzo]
Kwa kawaida huliwa baada ya kupikwa ingawa kuna aina zinazoliwa bichi pia kwa mfano karoti.
Majani mabichi[hariri | hariri chanzo]
Majani mengine huliwa bichi kama ni laini sana na ladha inapendeza yanaitwa saladi. Mchanganyiko wa nyanya, vitunguu na pilipili ni kachumbari. Saladi na kachumbari huongezwa mara nyingi mafuta, chumvi na asidi ya limau au siki kwa ladha.
Mboga kama chakula cha kando[hariri | hariri chanzo]
Mboga hutazamiwa kama sehemu ya chakula pamoja na ugali, ndizi au wali ambayo ni chakula cha kushibisha. Kutokana uzoefu huu wakati mwingine hata nyama huitwa "mboga" kwa maana ni chakula cha kando pamoja na ugali n.k.
![]() |
Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mboga kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |