Chainizi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chainizi (yaani "ya China", kutoka Kiingereza "Chinese leaf" au "Chinese cabbage"; jina la kisayansi: "Brassica rapa") ni aina ya mboga ya majani jamii ya kabichi za Ulaya. Kutoka China, ilipoanza kulimwa zamani sana, imeenea duniani kote.

Inatupatia afya katika miili yetu, hasa kwa sababu ina wingi wa vitamini A na C.

Mboga ya chainizi wakati wa kupikwa huwekwa vitu vifuatavyo: nyanya, kitunguu, karoti na pilipili hoho; hivyo ni vitu ambavyo huwekwa kwenye mboga ya chainizi.

Jinsi ya kupika mboga ya chainizi[hariri | hariri chanzo]

Kwanza kabisa unawasha moto wako wa mkaa au gesi. Ukimaliza unaweka sufuria yako kwenye jiko, halafu unaweka mafuta ila unaayaacha yapate moto kwanza. Yakipata moto unaweka kitunguu na unaacha mpaka kiwe cha kahawia. Ukishamaliza unaweka karoti unaacha mpaka iwe ya njano. Baada ya hapo unaweka pilipili hoho; ukisha weka hoho unaweka nyanya na unaacha zichemke kama dakika mbili. Ikisha chemka unaweka mboga yetu ambayo ni chainizi, unaikoroga kidogo, halafu unaacha ichemke kama dakika mbili. Baada ya hapo unatafuta chombo kizuri cha kuwekea mboga yetu. Hivo ndivyo mboga yetu inavyopikwa. Kaa tayari kula.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chainizi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.