Kabichi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Aina ya kabichi.

Kabichi (pia kabeji kutoka Kiingereza "cabbage") ni mboga yenye umbo la mviringo mkubwa na rangi ya kijani, nyekundu (zambarau), au nyeupe inayopandwa kwa msimu.

Kabichi inaweza kuliwa bada ya kupikwa au ikiwa mbichi naina manufaa mengi kwa afya. Kabichi ni juu ya thamani ya lishe.

Kichwa cha kabichi kwa ujumla huwa na kilo 0.5 hadi 4, na inaweza kuwa kijani, zambarau au nyeupe. Hadi mwaka 2012, kabichi nzito kabisa ilikuwa na kilo 62.71.

Kabichi inayoliwa na binadamu asili yake in kabichi mwitu. Kabichi ilianza kupandwa huko Ulaya kabla ya mwaka 1000 KK. Zilipofika Zama za Kati, kabichi ilikuwa sehemu kubwa ya vyakula vya Ulaya.

Kwa kawaida, vichwa vya kabichi huvunwa mwaka wa kwanza wa mzunguko wa maisha ya mmea huo, lakini mimea inayotengwa kwa ajili ya mbegu inaruhusiwa kukua mwaka wa pili.

Kabichi huathiriwa na upungufu wa virutubisho kadhaa, pamoja na kuliwa wadudu wengi, na kupatwa na magonjwa ya bakteria na ya vimelea.

Viungo vya njə[hariri | hariri chanzo]

Greentree.jpg Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kabichi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.