Nenda kwa yaliyomo

Kilogramu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kilo)
Nakala ya kilogramu asilia

Kilogramu ni kipimo sanifu cha SI kwa ajili ya masi ya gimba. Kifupi chake ni kg. Sehemu yake ndogo huitwa "gramu" kwa kifupi "g". Kuna gramu 1000 katika kilogramu moja. Hata kama kifizikia kuna tofauti kati ya masi na uzito kilogramu hutumiwa pia kama kipimo cha uzito.

Kilogramu moja ni sawa na masi ya kilogramu asilia ambayo ni kipande cha metali kilichopo mjini Paris kwenye Ofisi ya Kimataifa ya Vipimo. Nakala 40 za kilogramu asilia zilitengenezwa Paris na kutumwa penginepo duniani penye ofisi za kutunza vipimo kitaifa au kikanda.

Kilogramu ilikuwa kati ya vipimo vipya vilivyoanzishwa baada ya mapinduzi ya kifaransa pamoja na kipimo cha mita. Kiasili kilielezwa kuwa sawa na lita moja ya maji kwenye halijoto ya sentigredi 4 (kamili 3,98 °C). Lakini elezo hili halikuridhika wataalamu wa kimataifa wa vipimo wakaendelea kutengeneza mfano wake wa metali ya platini-iridi.

Nakala zake hutumiwa penginepo kuhakikisha mizani ya taifa fulani ni sahihi.

Siku hizi wataalamu wanatafuta bado njia bora kwa sababu wengi hawaridhiki kutegemea gimba moja ambalo linaweza kuharibiwa au kupotea.

  • kilogramu: 1 kg = gravu: 1 gv = gramu: 1000 g
  • kilogramu: 1000 kg = megagramu: 1 Mg = tani: 1 t
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kilogramu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.