Zama za Kati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Zama za Kati (pia Enzi ya kati) zilihusisha wakati wa katikati katika mgawanyo wa kitamaduni wa historia ya Ulaya katika “zama” tatu: ustaarabu wa

Kwa kawaida, Zama za Kati za Ulaya Magharibi huhesabiwa toka mwisho wa Dola la Roma ya Magharibi (karne ya 5) hadi kuanza kwa falme za kitaifa, mwanzo wa uvumbuzi wa ng’ambo ya Ulaya, kipindi cha mwamko-sanaa, na Matengenezo ya Waprotestanti kuanzia mwaka 1517. Mabadiliko haya yalionesha mwanzo wa kipindi cha Zama za Kisasa ambacho kilitangulia mapinduzi ya viwanda.

Caen Chato cheminronde.jpg

Zama za Kati hujulikana kama “Kipindi cha Mediavo”, au kifupi “mediavo” (mara nyingine hutamkwa mediaevo au kihistoria, medievo, Kiingereza Middle Ages).