Nenda kwa yaliyomo

Sukumawiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sukumawiki
(Brassica oleracea)
Mimea ya sukumawiki shambani
Mimea ya sukumawiki shambani
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Brassicales (Mimea kama kabichi)
Familia: Brassicaceae (Mimea iliyo na mnasaba na kabichi)
Jenasi: Brassica
Spishi: B. oleracea
L.
Kundi la kaltivari: Kundi Acephala

Sukumawiki (pia: sukuma wiki) ni aina ya kabichi isiyoumba 'kichwa' na inayoliwa sana katika Afrika ya Mashariki, hususa nchini Kenya. Inatengenezwa kwa kutumia majani mabichi yanayopikwa. Lakini sukumawiki inaweza kutengenezwa pia kwa kutumia aina nyingine za majani yanayofaa kupikwa.

Jina "sukuma wiki" lamaanisha ya kwamba hii ni njia ya kula kwa siku za wiki bila gharama kubwa hadi kufikia wikendi ambako chakula bora kinapatikana - kama pesa inatosha.

Huliwa mara nyingi pamoja na ugali au chapati. Nyama, samaki au karanga inaweza kuungwa mle.

Mfano wa upishi

[hariri | hariri chanzo]

Katakata majani. Chemsha vikombe viwili vya maji katika sufuria. Ongeza majani yaliyokatwa katika maji. Ongeza chumvi na viungo vingine kama maji ya limau, nyanya na kitunguu kilichokatwa.

Unaweza kuingiza pia vipande vya nyama, samaki na karanga.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]