Chapati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Upikaji wa chapati.
Chapati ya kawaida na chapati iliyokunjwa.

Chapati au Chapathi ni aina ya mkate ambao haukufura (inayojulikana kama roti) kutoka Bara Hindi. Matoleo yake hupatikana nchini Turkmenistan, katika nchi za Afrika Mashariki: Uganda, Kenya na Tanzania na katika Afrika Magharibi, na miongoni mwa nchi nyingine, Ghana.

Asili[hariri | hariri chanzo]

Chapati iliandikwa kwenye Ain-i-Akbari, hati ya karne ya 16, na Kiongozi wa Mughal aliyekuwa afisa wa Akbar, anayeitwa Abu'l-Fazl ibn Mubarak.

Ufafanuzi[hariri | hariri chanzo]

Kusukumwa kwa chapati.
Msichana kutoka jijini Mahakuta, India, akipika chapati ndani ya hekalu.

Ngano, ambayo ni mazao makuu Asia ya Kusini, ndiyo inayotumiwa. Chapati ni aina ya roti (mkate). Maneno haya mawili hutumika kwa kubadilishana mara nyingi. Roti ni jina la mkate wowote usiofura. Aidha, chapati ni aina ya roti iliyotokana na unga wa ngano na kupikwa kwenye tava (chombo cha kupikia kinachotumiwa kupikia chapati).

Upishi[hariri | hariri chanzo]

Chapati hutayarishwa kutoka unga (wa ngano) uliyokandwa, unga wa 'atta' kwa lugha ya Kiurdu / Hindi / Punjabi / Kibengali na maji. Baadhi ya watu pia huongeza chumvi pamoja na / au mafuta kwenye unga wa kukandwa. Sehemu ndogo ndogo ya donge la unga uliokandwa hukatwa na husukumwa kwa kutumia mpinimpaka iwe umbo la mviringo. Hili donge lililosukumwa huwekwa juu ya chuma cha kuchomea chapati na hupikwa kwa pande zote mbili. Katika baadhi ya mikoa, chapati hupikwa kwa muda mfupi juu ya chuma cha chapati, halafu huwekwa moja kwa moja juu ya moto mkali, ambayo inaifanya ifure kama puto. Ile hewa ya moto inaivisha chapati haraka kutoka kwa ndani. Katika baadhi ya maeneo ya kaskazini ya Uhindi (kama Punjab) na Pakistan, hii inaitwa phulka (yaani ambayo imefura).

Mara nyingi, chapati hupakwa siagi kwa juu. Kipande cha chapati hukatwa na hutumiwa kutolea kitoweo kama nyama au mboga iliyopikwa pamoja nayo. Pia, inaweza kukunjwa na kutumika kutolea vyakula vya majimaji kama dal.

Ukubwa wa chapati (kipenyo na upana) hutofautiana kulingana na maeneo tofauti tofauti au jiko tofauti tofauti. Katika jiji la Gujarat, kwa mfano, chapati inaitwa 'rotli' na inaweza kuwa nyembamba kama karatasi ya tishu. Chapati zinazopikwa katika jikoni mwa nyumba za kawaida huwa na kipenyo cha sentimita 15-18 kwa ajili 'tava' inayotumika hupimwa kwa upana unaotosheleza jiko la kawaida. Chombo cha kupikia chapati kilikuwa kikitengenezwa kutokamana na udongo, hapo zamani, lakini hivi sasa hutengenezwa kwa chuma. Aidha, kuna vyombo vinavyotumia stima nchini India. Umbo wa mpini inatofautiana kutoka kilingana na maeneo mbalimbali. Baadhi ya nyumba hutumia baraza za jikoni kwa kusukumia unga wa chapati, lakini nyumba nyingi hupenda kutumia bao la mviringo lililotengenezwa kwa mdao au jiwe kwa kusukumia chapati.

Chapati ni aina moja ya mikate mingi isiyofura itokayo nchini Asia Kusini. Roti, inayokandwa kama chapati lakini hupikwa kwenye tanuri, huitwa 'tandoori roti'. Mchanganyiko wa unga wa ngano na moja au zaidi ya ngano (kama chickpea, maise, au mtama) huitwa "missi roti". Roti hupikwa kwa kutumia mtama wa lulu (bajra) au mahindi (Makka) au (jowar) ma ni kawaida kutumia jina la unga, kama katika "bajra roti" au "makke ki roti". Mikate isiyofura kama chapati na roti ni vyakula vya jadi kaskazini ya nchi ya Asia ya Kusini. Pande za kusini, mashariki na kaskazini na bonde la Kashmir hula mchele kama chakula chao cha kitamaduni. Katika kusini mwa India, hakuna tofauti kati ya 'Chapati' na toleo la kukaangwa la 'paratha', ingawa sasa ya 'tandoori roti' ni hupatikana katika miji midogo midogo.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chapati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.