Tortilla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Utengenezaji wa tortilla
Tortilla ikijazwa nyama, kuku aum bgoga na kukunjwa huitwa "taco"

Tortilla ni aina ya mkate bapa wa Meksiko unaofanana na chapati. Kwa kawaida hutengenezwa kwa unga wa mahindi lakini siku hizi juna pia tortilla za ngano.

Wamexiko huandaa mahindi kwa kuipika katika maji walimotia kiasi cha chokaa na kuikoboa baadaye. Kupikwa katika chokaa kunaongeza lishe ya mahindi kwa sababu kuna proteini na vitamini ndani yake yasiyopokelewa na tumbo la kibinadamu bila maandalizi haya.

Sehemu kubwa ya kinyunga cha tortilla huandaliwa siku hizi viwandani na kuuzwa madukani. Kinyunga hiki hukaushwa tena na kusagwa ikiuzwa kwa umbo la unga utakaochanganywa tena na maji majikoni. Tortilla inaandaliwa kwa umbo la kisahani bapa kama chapati na kuokwa juu ya bati joto au kwenye sufuria.

Mboga wa kienyeji pamoja na tortilla ni maharagwe lakini kuna njia nyingi za kuzila.

Wengi wanapenda kula "taco" barabarani ambayo ni tortilla iliyojazwa nyama, kuku au mboga na kukunjwa ikiliwa mkononi.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tortilla kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.