Majadiliano:Tortilla

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Matamshi ya Tortilla[hariri chanzo]

kuhusu matamshi ya tortilla, ni kwamba "ll" kwa Kihispania cha Hispania inatamkwa "ly", ila katika Amerika ya Kilatini matamshi ni tofautitofauti, kwa mfano Kolombia ni "ja". Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:21, 8 Novemba 2019 (UTC) (mchango huu umehamiswa hapa kutoka majadiliano:tawimto)[jibu]

Asante, ni kweli unachosema kuhusu tofauti ya matamshi baina ya Hispania na Amerika ya Kilatini. Kwa hiyo je tuongeze njia zote mbili? Ila tu nasikia kwamba "tortilya" ya Hispania (inafanana na chipsi mayai) ni chakula tofauti na "tortiya" ya Meksiko ambayo ni chapati. Kipala (majadiliano) 09:29, 9 Novemba 2019 (UTC)[jibu]
Hiyo ni sahihi, na mimi nilipokuwa Hispania miaka 50 iliyopita nilifahamu hiyo ya huko. Ile ya Mexico nimejifunza kwako! Katika New World Encyclopedia nimepata maelezo zaidi. Mimi nafsi yangu naona katika ukurasa wa chipsi ingebaki ile ya Hispania, mradi ile ya Mexico ina ukurasa wake na sielewi kwa nini ichanganywe na chipsi ingawa haina viazi. Lakini si dogma! Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:34, 9 Novemba 2019 (UTC)[jibu]