Nenda kwa yaliyomo

Boga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maboga
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Maboga au malenge ni matunda ya mboga (pia mlenge) yenye umbo la kibuyu katika familia Cucurbitaceae. Matunda haya hutoka kwenye spishi mbalimbali katika jenasi Coccinia, Cucurbita na Momordica. Maboga huwa na rangi ya manjano, ya machungwa au ya majani na huwa na mikunjo kuanzia kwenye shina juu mpaka chini. Maboga yana kombe / ganda nene huku mbegu na nyama ya tunda ikiwa ndani.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Mbegu za Maboga (kukomaa)

Asili ya maboga haifahamiki vizuri japo yanasenekana kuanzia huko Amerika ya kaskazini ushahidi wa zamani kabisa ni ule wa maboga, zinazoonesha kuwepo tangu mwaka 7000 na 5000kk, zilizo patikana huko maksiko maboga huwa na saizi mbalimbali. kwanzia kilogramu 0.4 mpaka kilogram 453.

Shina la mmea wa maboga huwa gumu, lenye miba midogomidogo na lenye pembe tano. Kwa kawaida maboga huwa na uzito kuanzia kiligramu 4 mpaka 8, na kwa spishi ya (maxima inayoweza kufikia mpaka zaidi ya kilogramu 34.

Maboga huwa na ukubwa mbalimbali na umbo la muonekano mbali mbali vile vile japo kuwa maranyingi huwa na rangi ya njano., baadhi ya matunda huwa na rangi ya kijani (ya kukoza ama angavu), nyeupe, nyekundu na kijivu.

Mboga huwa sehemu za uzazi, kike na kiume katika mmea mmoja. Ua la kike hutofautishwa kwa ovary ndogo chini ya petali maua haya yenye rangi ingawa hudumu kwa muda mfupi sana, kama siku moja hivi rangi ya maboga hutokana na pigmenti za rangi ya njano zilizonyingi sana kwenye mmea huo.virutubisho muhimu ni mteini na karotini ambayo ni muhimu kwa kutengeneza vitamin A ndani ya mwili.


Mgawanyiko na makazi[hariri | hariri chanzo]

Maboga hukua maeneo mbalimbali ya dunia kutokana na sababu za kilimo ( kama vile kulisha wanyama) mpaka sababu za kibiashara na mapambo katika mabara yote saba. Ni bara la atrantiki pekee ndio hushidwa kuzalisha maboga wazalishaji wakubwa wa maboga duniani ni marekani, meksiko, india na china.


Ekolojia[hariri | hariri chanzo]

Kilimo cha maboga marekani kama ilivyo zao maalumu huko marekani kilogrammu ilioni 680 za maboga huzalishwa kila mwaka, majimbo yanayoongoza kuzalisha maboga huko marekani ni pamoja na Illinois, inainna, ohio, califania, na Pennsylvania, kulingana na idara ya kilimo ya illlinors, 95% ya maboga yanayofanyiwa utayarishaji wa ndani hutokea Illonois.

Maboga ni mazao ya msimu wa joto, ambayo hupandwa mwanzoni mwa mwezi julai, udongo unaotakiwa ni ule ambao kwa kina cha sm 7.62 iwe na joto la 155 c, na udongo unaotunza maji vyema maboga huweza kuzulika kama kukiwa na upungufu wa maji au kukiwa tu kuna joto dogo mno, na udongo ambao hauchuji maji vizuri, maboga hata hivyo ni magumu kwelikweli kama majani yake mengi yakiondolewa au kuharibiwa mmea unaweza kukua haraka na majani hukua tena haraka.kufidia yale yaliotolewa maboga huzalisha maua yote, ya kike na kiume nyuki hufanya kazi kubwa ya uchavushaji maboga yalifahamika kihistoria kuwa yanachavushwa na nyuki wa maboga (peporapis proinosa) lakini nyuki huwa wameadimika mno. Sasa kutokana na magonjwa mengi ya mimea na leo maboga wengi huchemswa na nyuki wa asali mzinga mmoja wa nyuki kwa ekali moja hushauriwa na idara ya kilimo ya marekani kama nyuki wakiwa wachache wakulima huchavusha kwa mikono yao wenyewe maboga yasiochavushwa ipasavo hasa kabla ya kukomaa. Fungi pia huhusika sana na hali hii.


Matumizi[hariri | hariri chanzo]

Mapishi[hariri | hariri chanzo]

Maboga yana matumizi mengi sana katika mapishi kuanzia ganda lake la nje mpaka mbegu, hata maua sehemu nyingi za maboga huliwa. Kwa kawaida na desturi maboga ni chakula zao maarufu sana kwennye sherehe ya watakatifu wote na siku ya shukurani ya mazao, ingawa wengi hununua kutoka madukani bado hata yale kutoka shambani huweza kufanya jukumu vilevile.

Kisha kukomaa, Maboga huchemswa, kuokwa, kupikwa kwa mvuke au hata kuchomwa. Huko amerika ya kaskazini na muhimu kwenye tamaduni zao ambao wakati wa mavuno ya kipupwe huchemsha na kunywa supu yake mwenyewe huko maksiko na marekani mbegu za maboga hukaanwa na kuliwa kama vitafunwa.


Dawa[hariri | hariri chanzo]

Chuo kikuu cha ‘East china normai ‘ kilifanya tafiti yake kwenye panya wenye kisukari, walio ichapisha julai 2007,’wakisema kuwa kikemikali zinazopatikana kwenye maboga huchangia uchangishwaji wa chembe seli za kongosho zilizo haribika na kupelekea kuongezeka kwa kiasi cha ishilni kwenye damu. Kulingana na kiongozi wa tafiti hiyo kemikali hizo zinaweza kuwa muhimu sana kwa mtu mwenye dalili za kwanza za kisukari na humwaidia tu yale mtu mwenye kisukari cha "type -1"


Mbegu[hariri | hariri chanzo]

Mbegu za maboga ni ndogo nyembamba na bapa zinazoweza kuliwa nyingi ya mbegu za maboga huwa na hupatikana kwenye maduka mengi mbegu za maboga zinafaida nyingi sana kiafya na hujumuisha kiwango kingi cha protini na vitamin na huaminika kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Gramu moja ya mbegu za maboga huwa na protini sawa na glasi moja ya maziwa, mbegu hizi pia huwa chanzo kizuri cha magnesium, manganisi, sosforasi na faitosterol’


Mafuta ya mbegu za maboga[hariri | hariri chanzo]

Mafuta ya mbegu za maboga huwa mekundu na mazito yanapotumika kupikia chakula kwa kawaida huchanganywa na mafuta mengine kwa sababu ya nguvu yake,yanatumika sana kupikia masahariki na kati mwa ulaya. Mafuta haya huaminika huwasaidia watu wenye matatizo ya tezi za uzazi, yaani "prostate". Mafuta haya pia huwa na kemikali zilizo saidia kuimarisha mishipa ya damu na mishipa ya fahamu.(neva) Matumizi mengine. Mara nyingi hushauriwa na wataalamu wa mifupa, kuwa maboga ni chakula kizuri kwa mbwa nap aka wanaopata matatizo ya umengenyaji wa chakula kiasi chake kingi cha makapi husaidia kuongeza na kuchochea mmengenyo wa chakula.