Matembele
Matembele ni majani ya viazi vitamu ambayo hutumika kama mboga kwa kuliwa na chakula na pia ina virutubisho vifuatavyo: Protini, Niacin, Calcium na madini ya chuma.
Jinsi ya kupika
[hariri | hariri chanzo]Andaa sufuria, nyanya, vitunguu, mafuta ya kula, pia andaa jiko la kupikia kama ni jiko la umeme, jiko la gesi au jiko la mkaa.
Kisha chambua matembele yako vizuri, katakata matembele yako kwa kisu, weka kwenye chombo cha kuosha, osha mara mbili au mara tatu kuondoa udogo au mchanga. Baada ya kuhakikisha mboga zako ni safi, kata vitunguu, kisha weka kwenye sufuria vitunguu vyako tayari kuanza mapishi. Washa jiko lako kisha weka sufuria uliyokatia vitunguu, tia mafuta ya kula kwenye sufuria. Baada ya hapo subiri kidogo vitunguu vyako viive; wakati unasubiri vitunguu viive katakata nyanya zako. Pia unaweza kuongeza viungo vingine kama vile karoti na pilipilihoho. Baada ya kuhakikisha umekata nyanya zako vizuri na viungo vingine, weka nyanya zako na viungo vingine kwenye kitunguu kinachoendelea kuiva, kisha koroga kupata mchanganyiko mzuri. Baada ya kupata mchanganyiko na rojo nzuri, weka chumvi, kisha weka matembele yako. Subiri dakika chache ili yaive. Yakishaiva, epua na hifadhi mboga yako kwenye chombo safi, tayari kwa kuliwa.
Watu wengine hupenda matembele yasiyo na viungo vingi, hupendelea kupika kwa kitunguu, chumvi na mafuta ya kula pekee.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Matembele kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |