Wakonjo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wakonjo katika mavazi ya kiasili

Wakonjo (au Wakonzo; kwa lugha yao: Bakonjo) ni kabila la Kibantu wanaoishi kwenye milima ya Ruwenzori, kusini magharibi mwa Uganda na kidogo upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo[1].

Mwaka 1992 walikadiriwa kuwa 362,000 hivi.

Lugha ya wengi wao ni Kikonjo, mojawapo kati ya lugha za Kibantu.

Tangu zamani ni wakulima, na kwa sasa wengi ni Wakristo.

Mwaka 2008 serikali imetambua rasmi Ufalme wa Rwenzururu, ulioundwa na Wakonjo pamoja na Waamba: ndio ufalme wa kwanza wa Uganda unaounganisha makabila mawili.[2]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Konjo: A language of Uganda", Ethnologue (accessed 7 June 2009)
  2. "Uganda: Welcome Rwenzururu", editorial by the New Vision, 31 March 2008
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakonjo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.