Robert Ouko
Dk. John Robert Ouko (maarufu kama ‘’’Robert Ouko’’’; 31 Machi 1931 - 13 Februari 1990) alikuwa mwanasiasa wa Kenya ambaye alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya. Ouko alihudumu katika serikali ya Kenya tangu wakati wa ukoloni chini ya Urais wa Jomo Kenyatta na Daniel arap Moi.
Alikuwa mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Kisumu Rural na pia alikuwa waziri wa maswala ya kigeni mnamo 1990.
Aliuawa nchini Kenya mnamo 13 Februari 1990. Kesi ya mauaji hayo haijawahi kusuluhishwa hadi sasa.
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Ouko alizaliwa katika kijiji cha Nyahera karibu na Kisumu, Mkoa wa Nyanza. Alihudhuria masomo katika Shule ya Msingi ya Ogada na Shule ya Upili ya Nyang’ori. Baada ya shule alisomea ualimu katika chuo cha Mafunzo ya Walimu cha Siriba. Alifanyakazi kama mwalimu wa Shule ya Upili.
Mnamo 1955 alipata ajira kama ofisa wa ushuru katika Wilaya ya Kisii. Mnamo 1958 alijiunga na Chuo Kikuu cha Haile Selassie Jijini Addis Ababa, Ethiopia, akifuzu kutoka huko mnamo 1963 na shahada katika kitengo cha ‘’Public Administration’’, Uchumi na Sayansi ya Siasa. Hatimaye alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda ambapo alisomea Diploma katika Kitengo cha International Relations and Diplomacy [1]
Kufikia kifo chake alikuwa karibu kumaliza Thesis ya shahada ya tatu ambayo alikuwa akisomea katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Licha ya kujulikana kuwa Dk. Ouko, alikuwa tu na shahada ya honorary ambayo aliipokea mnamo 1971 kutoka Chuo Kikuu cha Kilutheri cha Pacific
Maisha ya siasa
[hariri | hariri chanzo]Muda mfupi kabla ya uhuru wa Kenya mnamo 1963 alifanya kazi kama Katibu msaidizi katika ofisi ya Gavana. Punde alipandishw kuwa Katibu mkuu katika Wizara ya Kazi. Baadaya kuporomoka kwa Muungani wa Afrika Mashariki, Ouko aliteukiwa kuwa mbunge na akachaguliwa kuwa Waziri wa Mipango ya Kiuchumi na Maswala ya Kijamii[1]. Alichaguliwa kama mbunge katika Uchaguzi Mkuu wa 1979 kuwakilisha Jimbo la Uchaguzi la Kisumu Rural na akakihifadhi kiti hicho mnamo katika Uchagizi Mkuu wa 1983. Katika uchaguzi wa 1988 alihamia Jimbo la Uchaguzi la Kisumu Town (Baadaye liligawanywa kuwa Kisumu Town Mashariki na Kisumu Town Magharibi) na hapo alichaguliwa tena kama mbunge[2]. Ouko alikuwa akiwakilisha Chama cha KANU, ambacho kilikuwa chama pekee kilichokubaliwa na Sheria.
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Mnamo 27 Januari 1990, Ouko ambaye wakati huu alikuwa Waziri wa Nchi za Nje wa Kenya aliondoka Nairobi kama mmoja wa kundi la mawaziri 83 na maafisa, miongoni mwao akiwemo Rais Daniel arap Moi kuhudhuria mkutano wa ‘Kiamsha Kinywa cha Maombi’ ambao ulifanyika jijini Washington DC. Kikosi hicho kilirejea jijini Nairobi mnamo 4 Februari. Mnamo tarehe 5 Febuari, Ouko alikutana na rais Moi, balozi wa Japan, Kamishna mkuu wa Canada, Bethuel Kiplagat (Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Kigeni) na Hezekiah Oyugi (Katibu Mkuu wa Wizara ya Usalama wa Nchi). Baadaye siku hiyo Ouko alizuru nyumbani kwake mashinani katika shambalake lililoko Koru (Umbali wa takribani 300 km kutoka Nairobi) akiandamana na dereva wake na mlinzi.
Ouko alitoweka mnamo usiku wa 12 Februari/13, 1990 kutoka shamba lake la Koru karibu na Muhoroni Msaidizi wake wa nyumabani alitoa ushahidi kuwa aliisikia sauti kubwa kama ya kufungua mlango kwa nguvu ambayo ilimwamsha[3] na kuwa aliona gari jeupe likigeuka katika bustani ya kuendesha ya Ouko[4]. Maiti ya Ouko ilipatikana mnamo 13 Februari karibu saa saba mjana na kijana ambaye alikuwa akilisha, Joseph Shikulu katika eneo la chini la mlima ulioko karibu wa Got Alila, kilomita 2.8 kutoka myumbani kwa Ouko. Ushahidi kutokana na uchunguzi uliofanyiwa mwili ulionyesha kuwa alikuwa ameuawa kwa kupigwa risasi moja kichwani, mguu wake ukavunjwa mara mbili na mwili wake ukachomwa kwa kiasi kidogo.
Mwanzoni, ripoti za polisi ziliharifu kuwa Ouko alikuwa amejiua lakini hatimaye ilidhihirika kuwa alikuwa ameuawa na mwili wake kuchomwa.[5]. Msukumo wa wananchi ulimsukuma rais MOi kutafuta wapelelezi kutoka UK kuchunguza mauaji ya Ouko.
Zimeundwa kamati nyingi kuchunguza mauaji haya lakini suluhisho halijawahi kufikiwa.
Kamati Teule ya Bunge
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Mei 2003, Serikali iliyochaguliwa ya Mwai Kibaki ilifungua upya upelelezi wa mauaji ya Ouko. Upelelezi huu ungeekelezwa na kamati teule ya Bunge. Wakati wa shughuli za kamati hiyo, wabunge wengi waliishtumu hadharani kamati hiyo kwa njia ilivyoendeleza vikao vyake. Wengine walijing;atua kutoka kamati hiyo na pamoja na wengine waliobakia wakaapa kutoyaunga mkono matokeo ya Kamati hiyo.
Domenico Airaghi na Marianne Briner-Mattern walikubali kutoa ushahidi mbele ya kamati iwapo tu hawangeulizwa maswali ya upelelezi, (jambo ambalo walikuwa wamelikwepa wakati wa upelelezi wa awali wa Troon, uchunguzi wa wazi na upelelezi wa polisi) na Nicholas Biwott asikubaliwe kumtuma shahidi kwa niaba yake au kupeleleza mashahidi wengine.
Hata hivyo tume hiyo haikumaliza vikao vyake. Ilifutiliwa mbali mnamo 2005 kwa madai ya maingilio katika shughuli zake wakati Biwott alikuwa ameanza ushahidi wake. Kipengele cha Kamati hii teule hakikutajwa katika Bunge wala kupigiwa kura. [6] [7] [8]
Maisha ya binafsi
[hariri | hariri chanzo]Ouko alikuwa ameoa Christabel Ouko. Kifungua mimba wake anaitwa Ken [9]. Pia alikuwa na binti aliyezaliwa mnamo Mei 1983. Alimzaa binti huyu na hawara wake Herine Violas Ogembo, ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi naye hadi kifo chake (Ouko) [10].
Mnamo 2009, mchango ulifanywa kujenga maktaba ya Robert Ouko Memorial Community mjini Koru [1].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 Daily Nation, 4 Oktoba 2009: Ouko library a fitting tribute to ex-minister who loved books Archived 14 Septemba 2012 at the Wayback Machine.
- ↑ Center for Multiparty Democracy: Politics and Parliamenterians in Kenya 1944-2007 Archived 28 Februari 2008 at the Wayback Machine.
- ↑ Troon's Final Report paragraph 32
- ↑ Troon's 'Final Report' paragraph 33
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedpersist
- ↑ [1]
- ↑ [2]
- ↑ [3]
- ↑ The Standard, 8 Agosti 2009: Ouko family to construct a memorial library Archived 14 Agosti 2009 at the Wayback Machine.
- ↑ Troon's 'Final Report', paragraphs 120 to 124
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Cohen, David William & Odhiambo, E. S. Atieno (2004). The Risks of Knowledge: Investigations into the Death of the Hon. Minister John Robert Ouko in Kenya, 1990. Ohio University Press. ISBN 0-8214-1597-2.
Makala hii kuhusu mwanasiasa huyo wa Kenya bado ni mbegu. Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |