Zachary Onyonka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Zachary Onyonka

Zachary Onyonka (1938 - 2002) alikuwa Mwanasiasa wa Kenya. Alikuwa mbunge, akiwakilisha Jimbo la Uchaguzi la Kitutu Masaba.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Onyonka alizaliwa mnamo 1938 katika sehemu za Kisii nchini Kenya.

Ubunge[hariri | hariri chanzo]

Alichaguliwa mara ya kwanza kama mbunge wa Kitutu West wakati jimbo hili lilipoanzishwa mnamo 1969. Abakia kuwa mbunge wa Jimbo hili la uchaguzi hadi 1988 wakati jimbo hilo liligawanwa na kuzaa jimbo jipya la Kitutu Chache. Onyonka alikuwa mbunge wa jimbo hili jipya hadi kifo chake mnamo 2002.

Uwaziri[hariri | hariri chanzo]

Onyonka alihudumu kama Waziri wa Maswala ya Nji za Kigeni kati ya 1987 - 1988.

Kifo chake[hariri | hariri chanzo]

Aliaga dunia mnamo 2002 wakati angali akihudumu kama mbunge wa Kitutu Chache.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Jimbo la Uchaguzi la Kitutu Chache Jimbo la Uchaguzi la Kitutu Masaba

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

Alitanguliwa na
Elijah Mwangale
Waziri wa Nchi za Kigeni wa Kenya
1987-1988
Akafuatiwa na
Robert Ouko (Kwa mara ya Pili)

Kigezo:Mbegu-mwanasiasa-kenya