Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta
Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology - JKUAT) ni chuo kikuu cha umma kilicho karibu na jiji la Nairobi, Kenya. Chuo hiki kinapatikana mjini Juja, kilometa 36 Kaskazini Mashariki mwa Nairobi, katika barabara kuu ya Nairobi-Thika. Chuo hiki hutoa kozi katika Uhandisi, Sayansi, pamoja na Sanaa ya Uchoraji(Architecture) na Ujenzi (Construction). Chuo hiki kina nia imara ya utafiti katika maeneo ya teknolojia na uhandisi.
Historia
[hariri | hariri chanzo]JKUAT ilianzishwa mnamo mwaka 1981 kama Chuo cha Kilimo na Teknolojia (JKCAT), ambacho kilikuwa chuo cha kiwango cha katikati kilichoanzishwa na Serikali ya Kenya kwa msaada kutoka kwa Serikali ya Japani. Mipango ya kuanzisha JKCAT ilianza mnamo mwaka wa 1977. Mapema mwaka wa 1978, rais wa Kenya, Jomo Kenyatta, alichangia hekta mia mbili za shamba kwa ajili ya uanzishwaji wa chuo hicho.
Kundi la kwanza la wanafunzi lilisajiliwa mnamo tarehe 4 Mei 1981. Rais mpya Daniel Arap Moi alikifungua rasmi chuo cha JKCAT mnamo tarehe 17 Machi 1982. Sherehe ya kwanza ya mahafali ilifanyika Aprili 1984 huku vyeti vya Diploma vikikabidhiwa kwa wahitimu katika Uhandisi wa Kilimo,teknnolojia ya chakula na bustani.
Mnamo Tarehe 1 Septemba 1988, Daniel Arap Moi, alitangaza JKCAT kuwa Chuo husika cha Kenyatta University kupitia kwa Notisi ya kisheria, chini ya kifungu cha Sheria cha Kenyatta University (CAP 210C). Jina la JKCAT lilipadilishwa rasmi na kuwa Jomo Kenyatta University College of Agriculture and Technology (JKUCAT). Hatimaye kilifahamika kama Chuo Kikuu kupitia kifungu cha sheria JKUAT cha 1994 na kuzinduliwa rasmi tarehe 7 Desemba 1994.
Maendeleo
[hariri | hariri chanzo]JKUAT ni mwenyeji wa African Institute on Capacity Development (AICAD). Chuo hiki kinajulikana kuwa chuo kikuu zaidi cha teknolojia nchini Kenya. Wahandisi wanaofuzu kutoka chuoni humo hung'ang'aniwa na waajiri wanaposaka ajira. Kufikia sasa Chuo hiki kina kampasi nne. Tawi kuu liko Juja. Matawi mengine ni Nairobi Campus, Karen Campus na Taita Taveta Campus.