Majadiliano:Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ogeya Bphase made this verion (now redirects here):

JKUAT[hariri chanzo]

Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) ni chuo kikuu cha umma kilicho karibu na jiji la Nairobi, Kenya. Chuo hiki kinapatikana mjini Juja, kilomita 36 Kaskazini Mashariki mwa Nairobi, katika barabara kuu ya Nairobi-Thika Huwa yatoa kozi katika Uhandisi, Sayansi, pamwe na sayansi za Ujenzi. Chuo hiki kina nia imara ya utafiti katika maeneo ya teknolojia na uhandisi.


Historia[hariri chanzo]

JKUAT ilianzishwa mwaka wa 1981 kama Jomo Kenyatta Chuo cha Kilimo na Teknolojia (JKCAT), chuo cha kiwango cha wastani na Serikali ya Kenya kwa msaada kutoka kwa Serikali ya Kijapani . Mipango ya kuanzisha JKCAT yalianza mwaka wa 1977. Mapema mwaka wa 1978, rais wa Kenya, Jomo Kenyatta, alichangia hekta mia mbili za shamba kwa ajili ya uanzilishwaji wa chuo hicho.


Kundi la kwanza la wanafunzi walisajiliwa tarehe 4 Mei 1981. Rais mpya Daniel Arap Moi alikifungua rasmi chuo cha JKCAT mnamo tarehe 17 Machi, 1982. Sherehe ya kwanza ya mahafala yalifanyika Aprili 1984 huku vyeti vya shahada vikikabidhiwa kwa wahitimu katika Uhandisi wa Kilimo,teknnolojia ya chakula na bustani.


Mnamo Tarehe 1 Septemba, 1988, Daniel Arap Moi, alitangaza JKCAT kuwa Chuo husika cha Chuo Kikuu cha Kenyatta kupitia kwa Notisi ya kisheria, chini ya kifungu cha Sheria cha chuo kikuu cha Kenyatta (CAP 210C). Jina la JKCAT lilibadilishwa rasmi na kuwa Chuo cha wastani na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (Jomo Kenyatta University College of Agriculture and Technology), kwa ufupi JKUCAT. Hatimaye ilijulikana kama Chuo Kikuu kupitia kifungu cha sheria cha JKUAT, 1994 na kuzinduliwa rasmi tarehe 7 Disemba 1994.


Maendeleo[hariri chanzo]

JKUAT ni mwenyeji wa Taasisi ya Afrika juu ya Maendeleo ya Kiuwezo (African Institute on Capacity Development), AICAD.


Viunganish vya nje[hariri chanzo]