Joyce Banda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joyce Banda

Nchi Malawi
Kazi yake mwanasiasa

Joyce Hilda Banda (ukoo asili: Ntila; amezaliwa 12 Aprili 1950) ni mwanasiasa wa Malawi ambaye alikuwa Rais wa Malawi kutoka tarehe 7 Aprili 2012 hadi 31 Mei 2014.

Mwelimishaji na mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake, alikuwa Waziri wa Mambo ya nje kutoka 2006 hadi 2009 na Makamu wa Rais wa kwanza wa Malawi kuanzia Mei 2009 hadi Aprili 2012.

Banda alichukua madaraka kama Rais kufuatia kifo cha ghafla cha Rais Bingu wa Mutharika. Alikuwa Rais wa nne wa Malawi na rais wake wa kwanza wa kike na mkuu wa nchi wa pili wa kike baada ya Elizabeth II. Banda alikuwa mwanamke wa pili kuwa rais kwenye bara la Afrika. Alikuwa kiongozi mwenye maadili na hekima kubwa, ingawa aliwahi kuiingiza nchi yake na mzozo dhidi ya taifa la Tanzania mwanzoni mwa utawala wake.

Kabla ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Malawi, alikuwa akihudumu katika majukumu mbalimbali kama Mjumbe wa Bunge, Waziri wa Jinsia na Ustawi wa Watoto, na kama Waziri wa Mambo ya nje.

Kabla ya kazi yake katika siasa alikuwa mwanzilishi wa Joyce Banda Foundation, mwanzilishi wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wanawake wa Biashara (NABW), Mtandao wa Viongozi wa Vijana na Mradi wa Njaa.

Mnamo Juni 2014, Forbes alitaja Rais Banda kama mwanamke wa 40 mwenye nguvu zaidi duniani na mwanamke mwenye nguvu zaidi barani Afrika. Mnamo Oktoba 2014, alijumuishwa katika Wanawake 100 wa BBC.

Mnamo Novemba 2016, Banda alitangaza kuwa yuko tayari kusimama kama mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2019.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Joyce Banda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.