Nenda kwa yaliyomo

Saadani

Majiranukta: 6°02′36″S 38°46′48″E / 6.04333°S 38.78000°E / -6.04333; 38.78000
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

6°02′36″S 38°46′48″E / 6.04333°S 38.78000°E / -6.04333; 38.78000


Saadani
Saadani is located in Tanzania
Saadani
Saadani

Mahali pa Saadani katika Tanzania

Majiranukta: 6°2′40″S 38°46′38″E / 6.04444°S 38.77722°E / -6.04444; 38.77722
Nchi Tanzania
Mkoa wa Pwani
Wilaya ya Bagamoyo Kata ya Mkange
Boma la Kijerumani pale Saadani mnamo mwaka 2020

Saadani ni kijiji cha kata ya Mkange upande wa kaskazini wa Bagamoyo katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Saadani. Iko kwa mdomo wa Mto Mvavi (Mvave) kwenye ufuko wa Bahari Hindi.


Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kulikuwa mahali pa makazi ya Waswahili wa kale katika pwani ya kaskazini ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.

Kitovu cha biashara ya misafara

[hariri | hariri chanzo]

Katika karne ya 19 Saadani ilikuwa mji muhimu wa Waswahili na bandari kwa biashara ya misafara kwenda maeneo ya Tanganyika bara hadi Ziwa Tanganyika na Kongo.

Chini ya utawala wa Bwana Heri Saadani ilishindana na Bagamoyo juu ya nafasi kubwa katika biashara hiyo ya misafara.

Saadani ilishiriki katika vita ya Abushiri ikaharibiwa na manowari ya Wajerumani mwaka 1889 chini ya Hermann von Wissmann na kujengwa upya baada ya vita.

Kupotea kwa biashara

[hariri | hariri chanzo]
Soko jipya la Saadani.

Katika karne ya 20 biashara ya Saadani ilirudi nyuma hasa kwa sababu ilifaa kama bandari ya majahazi madogo tu lakini kina cha maji hakitoshi kwa meli kubwa zaidi. Meli ambazo sehemu zake za chini zilifikia mita 6 chini ya maji zilipaswa kukaa kilomita 6 mbele ya pwani.

Takwimu ya biashara ya mwaka 1908 ilihesabu meli 51 zilizofika mwaka huo lakini zilipaswa kukaa mbali na pwani na kuhamisha mizigo yake kwenye mashua na madhau. Pamoja na meli zilifika dhau 253. Thamani ya bidhaa zilizofika ilikuwa Mark milioni 0,314. Kufikia mwaka 1913 thamani hii ilishuka hadi milioni 0,066.

Baada ya Tanganyika kuwa chini ya Uingereza biashara ikakwama kabisa kwa sababu meli zilitumia tu bandari za kisasa za Tanga na Dar es Salaam.

Leo hii maghofu ya boma la Wajerumani bado yamesimama, majengo mengine ya kihistoria yamepotea, mawe yake yalitumiwa na wenyeji kwa ujenzi wao.

Karibu na ofisi ya Hifadhi ya Saadani kuna makaburi ya siku za Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ambayo hayatunzwi; zinazosomeka ni kaburi la mmisionari Mwingereza mmoja na kaburi la afisa ya forodha ya Kijerumani.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Saadani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.