Hifadhi ya Ruaha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hifadhi ya Ruaha

Hifadhi ya Ruaha iko katikati ya Tanzania umbali wa kilometa 131 magharibi kwa mji wa Iringa. Hifadhi ya taifa ya Ruaha inaenea kwa zaidi ya kilomita mraba 20,000 za ardhi. Hivyo ni mbuga ya pili kwa ukubwa Tanzania baada ya Hifadhi ya Taifa ya Nyerere (Selous).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi ya taifa ya Ruaha ilianzishwa na Wajerumani mnamo 1910 na mwanzoni iliitwa pori la akiba la saba. Mwishoni mwa miaka ya 1940, Waingereza waliochukua madaraka waliiita pori la akiba la Rungwa. Mnamo 1964, mwishowe iliitwa Hifadhi ya taifa ya Ruaha, kutokana na Mto Ruaha. Jina la Ruaha limetoholewa kutoka lugha ya Kihehe 'Ruvaha' likimaanisha 'mto', hii inamaanisha mto Ruaha Mkuu uliopita katikati ya hifadhi na ndio mto unaosaidia wanyama kupata maji mwaka mzima.

Wanyama na mimea[hariri | hariri chanzo]

Hifadhi ya Kitaifa ya Ruaha inajulikana kwa idadi kubwa ya tembo (inakadiriwa kuwa zaidi ya 10,000) wanaokusanyika katika eneo moja kuliko eneo lingine lolote Afrika Mashariki na idadi nzuri ya wanyama walanyama. Inajulikana sana kuwa moja ya hifadhi ambayo unaweza kuona makundi ya simba hadi simba 20. Pia ni eneo muhimu kwa mbwa mwitu.

Hifadhi hii ni maarufu kwa wanyama aina ya kudu wakubwa na wadogo ambao hupatikana kwa wingi katika hifadhi. Aina mbalimbali za samaki, viboko, na mamba hupatikana kwa wingi katika mto Ruaha. Wanyama kama pofu na swala pala hunywa maji katika mto Ruaha ambao ni mawindo ya kudumu kwa wanyama wanaokula nyama kama simba, chui, mbweha, fisi na mbwa mwitu.

Ruaha ni sehemu nzuri ya kuona ndege kuna aina zaidi ya 500 ya ndege (wote wa msimu na wa kudumu), Hifadhi ya Kitaifa ya Ruaha ni paradiso ya utalii wa ndege. Tena, anuwai ya ndege ni ya kushangaza, pamoja na ndege wa maji na wanyama wanaoruka kutoka kusini na kaskazini.[1].

Hifadhi hii ina sifa ya kuwa na wanyama na mimea karibu yote inayopatikana Kusini na Mashariki mwa Afrika.

Namna ya kufika[hariri | hariri chanzo]

Safari kwa kutumia ndege za kukodi kutoka Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Mbeya. Pia kupitia barabara.

Wakati mzuri wa kutembelea hifadhi hii na kuangalia wanyama wakubwa ni wakati wa kiangazi, kati ya mwezi Mei hadi Desemba. Kuangalia ndege na maua wakati wa masika (Januari hadi Aprili)

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Ruaha National park". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-01. Iliwekwa mnamo 2020-11-21. 

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Ruaha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.