Selous

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Hifadhi ya Selous (usemi: "saluu") ni hifadhi kubwa kuliko zote nchini Tanzania, pia ni kati ya hifadhi kubwa kabisa ya wanyama duniani.

Eneo lake ni la km² 54,600 katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Eneo hilo ni kubwa kushinda nchi 70 duniani ikikadiriwa kuwa na eneo sawa na nchi ya Kostarika (Amerika ya Kati) na takribani ukubwa mara mbili ya nchi ya Ubelgiji (Ulaya).

Tangu mwaka 1982 imeingizwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia. Mwezi Juni 2014 iliingizwa kwenye orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia miongoni mwa hifadhi zenye hatari ya kupoteza uhai wake.

Jina limetokana na Mwingereza Frederick Selous aliyekuwa mwindaji wakati wa kuanzishwa kwa ukoloni katika Afrika ya Kusini na Mashariki na ambaye aliuawa katika Tanzania ya leo akiwa mwanajeshi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Sehemu kubwa ya eneo iko katika hali ya asili bila kuvurugwa na shughuli za binadamu. Kuna wanyama kama tembo, kifaru, simba, twiga, kiboko na mamba.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]