Urithi wa Dunia
Urithi wa Dunia ni maeneo yenye thamani kubwa ya kiutamaduni au kimazingira duniani yanayoangaliwa na shirika la UNESCO.
Hadi Julai 2019 sehemu 1,121 katika nchi 167 zimekubaliwa. Nchi zinazoongoza kwa wingi wa mahali ni Italia na China zenye 55 kila moja, zikifuatwa na Hispania (48), Ujerumani (46) na Ufaransa (45).
Afrika ina mahali 96 (8.56%).
Orodha rasmi ya UNESCO ina mahali 869 pa urithi wa dunia wa kiutamaduni na mahali 213 pa urithi wa dunia wa kimazingira, mbali ya 39 pa mseto.
Mwanzo wa jitihada za kuhifadhi urithi wa dunia ulikuwa ujenzi wa bwawa la Assuan lililoelekea kuzamisha majengo mbalimbali ya utamaduni wa Misri na Nubia wa kale chini ya maji. Wakati ule UNESCO ilifaulu kukusanya pesa ili hekalu la Abu Simbel liweze kuhamishwa mlimani kabla ya kujaa kwa bwawa.
Tangu 1972 kuna mkataba wa kimataifa wa Stockholm kuhusu hifadhi ya urithi wa dunia kiutamaduni na kimazingira.
Kila mahali panapopendekezwa ili pakubaliwe panahitaji angalau sifa moja kati ya sita zifuatazo:
- kuwa na thamani ya pekee ya kisanii
- kuwa na athira muhimu katika eneo fulani au kipindi cha historia
- kuwa kitu cha pekee kisichopatikana tena au kuwa na umri mkubwa
- kuwa mfano bora wa kipindi fulani cha historia ya ujenzi
- kuwa muhimu katika uhusiano na fikra muhimu au watu muhimu wa historia
Kamati ya Urithi wa Dunia hukutana kila mwaka na kuangalia maombi ya kupokelewa katika orodha ya urithi wa dunia. Kamati inapokea taarifa kuhusu hifadhi na hali ya urithi uliopo tayari orodhani. Kila baada ya miaka miwili orodha inatolewa upya.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
UNESCO World Heritage List travel guide kutoka Wikisafiri
Kigezo:Library resources box
- UNESCO World Heritage portal – Official website (in English and French)
- The World Heritage List – Official searchable list of all Inscribed Properties
- KML file of the World Heritage List – Official KML version of the list for Google Earth and NASA Worldwind
- UNESCO Information System on the State of Conservation of World Heritage properties – Searchable online tool with over 3.400 reports on World Heritage sites
- Official overview of the World Heritage Forest Program
- Convention Concerning the Protection of the World Cultural and Natural Heritage – Official 1972 Convention Text in 7 languages
- The 1972 Convention at Law-Ref.org – Fully indexed and crosslinked with other documents
- Protected Planet — View all natural world heritage sites in the World Database on Protected Areas
- World Heritage Site – Smithsonian Ocean Portal
- Time magazine. The Oscars of the Environment – UNESCO World Heritage Site Archived 24 Agosti 2013 at the Wayback Machine.
- UNESCO chair in ICT to develop and promote sustainable tourism in World Heritage Sites
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |