Nenda kwa yaliyomo

Google Earth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Google Earth
Mwandishi wa kwanzaKeyhole, Inc.
Wandishi wa sasaGoogle
Tarehe ya kwanza28 Juni 2005 (as Google Earth)
circa 2001 (as EarthViewer 3D)
Imeendelea5.1.3533.1731 / Novemba 18, 2009; miaka 14 iliyopita (2009-11-18)
Toleo ya onyesho jipyaNone
Mfumo wa uendeshajiWindows 2000, XP & Vista, Mac OS X, iPhone OS, Linux
Ukubwa wa faili10 MB (8.9 MB iPhone; 24 MB Linux; 35 MB Mac )
Lugha41 languages, see the full list
Aina ya programuVirtual globe
Leseni ya programuFreeware/Proprietary
Tovutihttp://earth.google.com/

Google Earth ni programu ya habari kuhusu dunia isiyokuwa bayana , ramani na habari ya kijiografia ambayo awali iliitwa EarthViewer 3D, na iliundwa na Keyhole, Inc, kampuni iliyonunuliwa na Google mwaka wa 2004. Inatengeza ramani ya dunia kwa kupachika picha zilizopatikana kutoka kwa picha za satelaiti, picha za angani na za pande 3 za GIS. Inaendeshwa kwa leseni tatu tofauti: Google Earth, toleo lisilolipiwa na lililo na uwezo mdogo wa utekelezaji; Google Earth Plus (ilisimamishwa) [1] [2] ambayo ina matumizi zaidi; na Google Earth Pro ($ 495 kwa mwaka), ambayo imelengwa kwa matumizi ya kibiashara. [3]

Huduma hii, ambayo ilizinduliwa kama Google Earth mwaka wa 2005, hivi sasa inapatikana kwa matumizi katika kompyuta za kibinafsi zilizowekwa programu za Windows 2000 au zaidi, Mac OS X 10.3.9 na zaidi, Linux Kernel: 2.4 au toleo la baadaye (lililotolewa tarehe 12 Juni 2006) , na FreeBSD. Google Earth inapatikana pia kama {0 kisakuzi kiunganishi} ambacho kilizinduliwa tarehe 28 Mei 2008 [4] Ilianza pia kupatikana kwenye iPhone OS 27 Oktoba 2008, bila malipo kutoka hifadhi ya programu. Mbali na kuibua programu zilizoiimarishwa na Keyhole, Google pia iliongeza picha kutoka kwa hifadhidata yake ya Dunia, kwa programu yao ya kutengeza ramani. Mfunguo wa Google Earth Juni 2005 kwa umma ulisababisha ongezeko mara dufu la kuangaziwa na vyombo vya habari dunia isiyokuwa bayana kati ya 2005 na 2006, [5] kuhamasisha umma kuhusu teknolojia na programu ya setilaiti ya kukagua dunia.{0(}

Muhtasari

[hariri | hariri chanzo]

Google Earth huonyesha picha za setilaiti za uangavu tofauti za sura tofauti tofauti ya Dunia, jambo linalowawezesha watumiaji kuona vitu kama miji, nyumba, kutoka juu au kwa upande hanamu, (tazama pia mtazamo wa wa kutoka angani). Kiwango cha uangavu kinachopatikana kinategemea sifa zinazopendeza na umaarufu, lakini sehemu kubwa ya dunia(isipokuwa baadhi ya visiwa)zimefunikwa angalau katika mita 15 za uangavu. [6] Melbourne, Victoria, Australia; Las Vegas, Nevada; na Cambridge, Cambridgeshire ni mifano yenye uangavu wa juu sana, wa sentmita 15 ( nchi6). Google Earth inaruhusu watumiaji kutafuta anwani kwa baadhi ya nchi, kuingia anaratibu, au tu kwa kutumia puku kusakura hadi mahali.

Kwa sehemu kubwa ya uso wa dunia picha za pande 2 tu ndizo zinapatikana, kutoka upigaji picha wa karibu wima. Ukitazama kutoka upembe, kuna mtazamo kwa maana kwamba vitu ambavyo viko mbali kwa mlalo vinaonekana vikiwa vidogo, lakini bila shaka ni kama kutizama picha kubwa, sio kabisa kama mtazamo wa pande 3.

Kwa maeneo mengine ya uso wa dunia picha za pande 3 za Mandhari na majengo zinapatikana. Google Earth inatumia data ya digital elevation model (DEM) zilizokusanywa kwa mtambo wa NASA waShuttle Radar Topography Mission (SRTM). Hii ina maana mtu anaweza kutazama Grand Canyon au Mlima Everest katika pande tatu, badala ya pande 2 kama maeneo mengine. Tangu Novemba 2006, mitazamo ya pande 3 ya milima mingi, ikiwemo mlima Everest, imeboreshwa kwa kutumia data za DEM kujaza mapengo katika habari ya SRTM. [7]

Watu wengi hutumia programu kuongeza data zao wenyewe, kwa kuzifanya kupatikana kupitia vyanzo mbalimbali, kama vile Bulletin Board Systems (BBS) au blogu zilizotajwa katika sehemu ya viungo hapo chini. Google Earth inaweza kuonyesha kila aina ya picha zikiwa zimepachikwa juu ya uso wa dunia na pia ni programu ya Web Map Service. Google Earth inasaidia katika kuratibu data ya satelaiti ya kukagua dunia kwa kupitia Keyhole Markup Language{0{/0} (KML).

Google Earth ina uwezo wa kuonyesha picha za pande 3 za majengo na miundo (kama vile madaraja), ambayo inajumuisha michoro iliyowasilishwa na watumiaji kwa kutumia SketchUp, ambayo ni programu ya kutengeza vielelezo katika pande 3. Katika matoleo awali ya Google Earth (kabla ya toleo la 4), majengo ya pande 3 yalikuwa yanapatikana katika miji michache , na yalionekana vibaya, bila umbo. Majengo na miundo mingi Duniani sasa ina miundo naganaga ya pande 3; zikiwemo (lakini siyo tu ) Marekani, Canada, Ireland, India, Japan, Uingereza, Ujerumani, Pakistan na miji ya, Amsterdam na Alexandria. Katika Agosti 2007, Hamburg ukawa mji wa kwanza kuonyeshwa kabisa katika pande 3, pamoja na umbo kama gao. {0Mji wa Westport{/0} wa Ireland uliongezwa kwa Google Earth katika pande 3 mnamo 16 Januari 2008. Kielelezo cha 'Westport3D' kiliundwa na kampuni ya kuchukua picha za pande 3 ya, AM3TD kwa kutumia teknolojia aina ya leza ya kulenga mbali na kuchukua picha za dijitali na ni kielelezo cha kwanza cha mji wa Ireland kuundwa. Kwa vile awali iliundwa ili kusaidia Serikali ya Mtaa katika kuendesha kazi ya kupanga mji inajumuisha mfumo wa kupiga picha za kipekee za kuaminika zenye uangavu wa hali ya juu sana kuwahi kupatikana katika Google Earth. Picha za pande tatu za majengo na miundo zinapatikana kote duniani kupitia hifadhi ya picha za pande 3 za Google [8] na tovuti nyingine.

Majuzi, Google iliongeza kipengele kinachoruhusu watumizi kutazama mbio za magari katika vizuizi vilivyo yadi 200 katika wakati halisi. Katika toleo la 4.3 lililozinduliwa 15 Aprili 2008, kifaa cha kukuzia picha cha Google Street View kiliunganishwa kikamilifu katika programu na kuiwezesha programu hiyo kutoa mtazamo wa kiwango cha mtaani katika maeneo mengi.

Tarehe 17 Januari 2009, picha zote za Google za sakafu ya bahari zilitengenezwa upya na SIO, NOAA, jeshi la wanamaji la US , NGO, na GEBCO. Picha hizo mpya zimesababisha visiwa vidogo kama vile vya Maldives, kutoweza kuonekana licha ya kuwa fuo zao zimelainishwa kabisa. [9]

Tarehe 21 Oktoba 2009, picha za eneo zima la Poland zilitengenezwa upya (sehemu nyingi zilitatiza kuonekana katika uangavu wa chini, sasa zimeshatengenezwa upya), na - katika maeneo mengine - zimeshushwa (katika uangavu mzuri sana, sasa ni wa kadri).

Tangu toleo la 5.0 Google Earth inapatikana katika lugha 37 (nne kati ya lugha hizo zina lahaja mbili):

width = "33%" valign = "top" width = "33%" valign = "top" width = "33%" valign = "top"

Vipengele

[hariri | hariri chanzo]

Wikipedia na muunganisho wa Panoramio.

[hariri | hariri chanzo]

Desemba 2006 Google Earth iliongeza safu mpya inayoitwa "Geographic Web" inayojumuisha kuiunganisha na Wikipedia na Panoramio. Katika Wikipedia, viingilio vinachunguzwa kuona kama vina nambari tambulizi kupitia Coord templates Pia kuna safu ya jamii kutoka mradi wa Ulimwengu wa Wikipedia. Nambari tambulizi zaidi hutumiwa, aina tofauti ziko katika kionyesho na lugha mbalimbali zinasaidiwa kuliko safu ya ndani ya Wikipedia. Angalia: *safu inayobadilika resp. isiyobadilika. Google ilitangaza tarehe 30 Mei 2007 kuwa inainunua Panoramio. [10]

Kiigiza Kupepea

[hariri | hariri chanzo]

Tangu Google Earth v4.2, kiigiza kupepea kimejumuishwa kama kipengele kilichofichika. Kutegemeana mfumo,kinaweza kupatikana kwa kubonyeza Control + Alt + A, Control + A, au Command + Chaguo + A.Baada ya kipengele hiki kuwezeshwa angalau mara moja, kinaonekana chini ya menu zana. Tangu v4.3 chaguo hilo si siri tena. Sasa F-16 Fighting Falcon na Cirrus SR-22 ndizo ndege pekee ambazo zinaweza kutumika, na viwanja vichache vya ndege. [11] Pia inawezekana kudhibiti kiigiza kwa puku au kifaa cha joystick, ingawa si miundo yote inayowezeshwa kwa sasa.

Kiigiza kupepea cha Google Earth kinajumuisha uwezo wa kupaa hadi maeneo yoyote yaliyowezeshwa duniani. Rubani anaweza kuchagua mahali popote kuanzia kupepea au ajaribu kutua popote duniani. Muda wa kupaa si wa kasi sana, kwani F-16 ikiwa katika kasi ya juu kabisa angalau huchukua dakika 60 kuruka kutoka ufuo hadi ufuo mwingine wa Marekani kwa kutumia ndege hiyo. Ndege inaweza kutua mahala popote tambarare duniani (pamoja chini ya bahari katika Google Earth 5,0) iwapo kasi ya ndege ni chini ya 250 knots na inaanguka kwa kasi chini ya m 610 (ft 2 000) kwa dakika inapogusa ardhi.

Ndege husika

[hariri | hariri chanzo]
 • F-16 Fighting Falcon - Kasi ya juu na upeo mrefu kuliko Cirrus SR-22, ina uwezo wa kuruka kwa kasi za karibu 1300 knots katika upeo ulio karibu sana na ardhi. [onesha uthibitisho]
 • Cirrus SR-22 - Ingawa ina mwendo wa kasi wa chini kiasi na upeo wenye urefu mfupi kiasi, SR-22 ni rahisi kushughulikia na inapendelewa kwa utazamaji wa karibu kwa kutumia upigaji picha wa Google Earth.

Hali ya Angani

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu: Google Sky

Google Sky ni kipengele kilichoanzishwa katika Google Earth 4.2 mnamo 22 Agosti 2007, na kinawaruhusu watumiaji kutazama nyota na miili mingine ya mbingu. [12] Ilitengezwa na Google kwa ushirikiana na Space Telescope Science Institute (STScI) kutoka Baltimore, kituo cha sayansi ya Darubini ya Hubble Space. Daktari Alberto Conti na mtengeza mwenza Daktari Carol Christian wa STScI wana mpango wa kuongeza picha za umma za 2007, [13] pia picha za rangi zilizohifadhiwa za Hubble's Advanced Camera for Surveys. Picha zilizotolewa karibuni kutoka picha za Hubble zitaongezwa kwa programu ya Google Sky haraka kama zinavyotolewa. Vipengele vipya kama vile data yenye masafa mengi, mahali setilaiti zilipo na njia zao, vilevile rasilimali za elimu zitatolewa kwa jamii ya Google Earth pia kwa tovuti ya Christian na Conti ya website for Sky. Pia inayoonekana katika hali ya angani ni mpangilio wa nyota, nyota, mkusanyiko wa nyota na mifano kwa michoro inayoonyesha sayari na mizunguko yao. Google Sky ya wakati-halisi ni mchanganyiko wa muda mfupi wa angani wa karibuni, kwa kutumia itifaki yaVOEvent, inayotolewa na ushirikiano wa VOEventNet Archived 6 Machi 2015 at the Wayback Machine.. Ramani za Google Earth zinatayarishwa upya kila dakika 5.

Google Sky inapata ushindani [14] kutoka kwa Microsoft Worldwide Telescope (ambayo inaendeshwa tu kwa programu inayoendesha kompyuta ya Microsoft Windows) na kutoka Stellarium (programu ya kompyuta), programu huru na ishara wazi ya usayari inayoendeshwa na programu zinayoendesha kompyuta za Microsoft Windows, Mac OS X, na Linux.

13 Machi 2008, Google ilitoa toleo la Google Sky linalopatikana katika tovuti ya http://www.google.com/sky/.

Street View

[hariri | hariri chanzo]
Makala kuu: Google Street View

Tarehe 15 Aprili 2008 kupitia toleo la 4.3, Google iliunganisha kikamilifu Street View ndani ya Google Earth.

Google Street View inatoa mtazamo wa 360 ° wa mtaani na inawaruhusu watumiaji kutizama sehemu teule za miji na maeneo ya karibu katika usawa wa ardhi. Wakati ilizinduliwa tarehe 25 Mei 2007 kwa ajili ya Ramani za Google, ni miji mitano tu ilijumuishwa. Kwa sasa imepanuliwa kufikia zaidi ya miji 40 ya Marekani, na inajumuisha vitongoji vya miji mingi, na katika baadhi ya matoleo, miji mingine ya karibu. Matoleo ya hivi karibuni yametekeleza 'Street View' katika miji mingi mikubwa ya Australia na New Zealand vile vile sehemu za Canada, Ujapani, Uhispania, Ufaransa, Uingereza, Uholanzi, Italy, Uswisi, Ureno, na Taiwan.

Google Street View, inapofanya kazi, huonyesha picha zilizopigwa awali na kamera iliyoko juu ya gari, na zinaweza kutizamwa kwa kutumia puku ili kubonyeza picha zinazoonyeshwa kwenye kisetiri katika mwelekeo wako wa kusafiri. Kwa kutumia vifaa hivi, picha huweza kutazamwa katika ukubwa tofauti, kutoka upande wowote, na kutoka pembe mbalimbali.

Ilianzishwa katika toleo 5.0 (Februari 2009), kipengele cha Google Ocean/0} kinaruhusu watumiaji kutizama chini ya usawa wa bahari na kuangalia kipengele cha tatu cha pande 3 chini ya mawimbi. Inaendesha zaidi ya safu 20 ya maudhui, ina taarifa kutoka wanasayansi na wasomi wa bahari mashuhuri. [15] Tarehe 14 Aprili 2009, Google iliongeza data ya mandhari chini ya maji kutoka kwa Maziwa Makuu. [16]

Picha za Kihistoria

[hariri | hariri chanzo]
Faili:Ziggurat 1993-2009.JPG
Ulinganifu wa upande kwa upande wa Ziggurat na Raley Field Sacramento Magharibi, California kuanzia 1993 upande wa kushoto na 2009 upande wa kulia. Kama inavyoonekana katika upande wa 1993, Raley Field na Ziggurat hazipo.

Baada ya kuanzishwa katika toleo 5.0, picha za kihistoria zinaruhusu watumizi kurudi nyuma katika wakati na kujifunza hatua za awali za mahali. Kipengele hiki ni muhimu sana kwa madhumuni ya utafiti ambao unahitaji uchambuzi wa zamani wa kumbukumbu mbalimbali. [17]

Makala kuu: Google Mars
Faili:Google Mars R Osman.jpg
Mtazamo wa uangavu wa juu wa Victoria Crater unaoonyeshwa katika pande 3 kutumia kipengele cha Mirihi katika Google Earth 5

Google Earth 5 inajumuisha tufe ya sayari ya Mirihi, ambayo inaweza kutazamwa na kuchambuliwa kwa madhumuni ya utafiti. Ramani hizi ni za uangavu wa juu sana kuliko za toleo la Google Mars za kisakuzi na pia inaonyesha picha za pande 3 za Mandhari ya Mirihi. Pia kuna baadhi ya picha ambazo zina uangavu wa juu sana kutoka kwa kamera za HiRISE kwenye chombo cha Mars Reconnaissance Orbiter picha zenye uangavu wa juu kama za miji mingine duniani. Hatimaye, kuna picha nyingi za kutoka kwa vifaa vilivyotua katika sayari ya Mirihi, kama vile Mars Exploration Rovers, Spirit and Opportunity, ambazo zinaweza kutazamwa katika njia inayofanana na ya Google Street View. Linalovutia ni kwamba, safu ya juu ya Google Earth (idadi ya watu wanaoishi mahali duniani) inaweza pia kutumika kwa Mirihi. Safu za Mirihi pia zinaweza kutumika kwenye dunia.

Makala kuu: Google Moon
Faili:Google moon 1.jpg
Mojawapo ya mitambo inayotua mwezini kutazamwa katika Google Moon

Mnamo, tarehe 20 Julai 2009, wakati wa maadhimisho ya mwaka wa 40 wa misheni ya Apollo 11, Google ilianzisha toleo la [[Google{ Moon/0}]] [18] ambalo linaruhusu watumiaji kutazama picha za setilaiti za Mwezi. Ilitangazwa na kuonyeshwa kwa kundi la wageni waalikwa na Google pamoja na Buzz Aldrin kwenye Newseum huko Washington, DC. [19] [20]

Vishawishi

[hariri | hariri chanzo]

Kusano ya Google Earth inafanana na programu ya"Earth" iliyoelezwa na Neal Stephenson katikaSCI-fi classic Snow Crash. Hakika, mwanzilishi mwenza wa Google Earth alidai kuwa Google Earth iliundwa kwa mfano wa Snow Crash, [21] wakati mwanzilishi mwenza mwingine alisema ilitokana na filamu fupi ya elimu ya sayansi ya Powers of Ten. [22] Kwa kweli Google Earth kwa kiasi ilizaliwa kutokana na onyesho la Silicon Graphics liitwalo "From Space to in Your Face" ambalo lilisogea kutoka angani hadi ndani ya mlima wa Swiss Alps hadi Matterhorn [23] Onyesho hili la uzinduzi liliandaliwa na Onyx 3000 iliyo na grafiki InfiniteReality4 [24], ambayo iliwezesha Clip Mapping na ilitokana na vifaa vilivyowezesha kuweka picha kwa mfumo (ingawa haikutumia Clip Mapping) na "Powers of Ten". Utekelezaji wa kwanza wa Google Earth unaoitwa Earth Viewer uliibuka kutoka Intrinsic Graphics kama onyesho la matekelezo ya programu ya Chris Tanner iliyotegemea mfumo wa kuweka picha zaidi ya moja na utumizi wa picha kama ramani, na ulitokana na Keyhole Inc. Earth Viewer ilikuwa ni utambuzi wa hali ya juu ya uwezo wa mwungo wa mfumo wa kuweka picha za aina moja na wengi wa watu waliofanya kazi katika mradi wa Earth viewer walikuwa wamefanya kazi na Silicon Graphics.

Maelezo ya Kiufundi

[hariri | hariri chanzo]

Maelezo mengi ya toleo/ historia /logi ya mabadiliko yanapatikana kwa Google. [25]

Picha na uratibu

[hariri | hariri chanzo]
 • Kuratibu mfumo na makadirio
  • Mfumo wa ndani wa ratibu ya Google Earth ni nambari tambulizi za kijiografia (Latitudo / Longitudo) katika mfumo wa World Geodetic System wa 1984 (WGS84).
  • Google Earth inaonyesha ulimwengu ulivyo kama unavyoonekana kutoka jukwaa lililoinuka kama ndege au setilaiti inayozunguka. Mwinuko unatumika kufikia athari hii unaitwa Mtazamo wa Kawaida. Hii ni sawa na kukiwakilisha kitu chenye pande tatu kwa kutumia pande mbili, isipokuwa mahali pa kutazamia ni urefu unaoweza kukadiriwa (karibu na ardhi) badala ya umbali usio weza kukadiriwa(anga yenye kina kirefu).
 • Uangavu wa kimsingi
  • Jamhuri ya Chek: 0.5 m (ya Eurosense / Geodis Brno)
  • Slovakia: 0.5 m (ya Eurosense / Geodis Slovakia)
  • Hungaria: 2.5 m picha za SPOT (inaweza chukuliwa kuwa: 0.5 m (ya Eurosense / FÖMI)
  • Ujerumani, Uswisi, Uholanzi, Denmark, Uingereza, Andorra, Luxemburg, Liechtenstein, San Marino, Mji wa Vatikan: 1 m au zaidi
  • Balkan: 2.5 m (uangavu wa wastani)
  • Marekani: 1 m (isipokuwa Alaska & Hawaii)
  • Global: kwa ujumla 15 m (baadhi ya maeneo, kama vile Antaktica, yako katika uangavu wa chini sana), lakini hii hutegemea ubora wa picha za setilaiti / picha ya angani iliyopakiwa.
 • Uangavu wa Juu
 • Uangavu wa Muinuko:
  • Uso: unategemea nchi nchi
  • Sakafu ya Bahari: Haikuwa ikihusika awali, lakini tangu kuanzishwa kwa "Ocean", data ya mwinuko imeanzishwa (skeli ya rangi inayokadiria kina cha sakafu ya bahari 'inachapishwa' kwenye uso wa mdwara kutoka mtazamo wa miinuko ya juu).
 • Umri: Tarehe za picha zinatofautiana. Data ya picha inaweza kuonekana kutoka kwenye miraba inayotengezwa wakati 'DigitalGlobe Coverage' imewezeshwa. Tarehe iliyo kando ya habari ya hakimiliki si tarehe sahihi ya picha. Kuvuta ndani au nje kunaweza kubadili tarehe ya picha. Nyingi ya picha za kimataifa za mijini ni za mwaka wa 2004 na hazijaongezewa habari mpya. Hata hivyo, picha za Marekani zinaongezwa habari mara kwa mara. Google hutangaza wanapoongeza habari kwenye picha zao kupitia blogu yao ya LatLong [26] kwa kuuliza maswali yenye vidokezo kuhusu mahali palipoongezewa. Majibu yanawekwa kwenye blogu hiyo baada ya siku kadhaa.

Vifaa na programu

[hariri | hariri chanzo]

Google Earth haiwezi kufanya kazi kwa vifaa vyenye muundo wa zamani. Pakua za karibuni zinazopatikana Archived 11 Machi 2009 at the Wayback Machine. zinaonyesha miundo ya chini ifuatayo:

 • Pentium 3, 500 MHz
 • 128 MB RAM
 • 12.7 MB nafasi wazi kwenye disk (400 MB kwa Linux)
 • Kasi ya mtandao: 128 Kbit/s
 • kadi ya grafikiya 16MB yenye uwezo wa kuonyesha pande 3
 • Uangavu wa 1024x768, Rangi ya Juu ya 16-bit
 • Windows XP au Windows 2000, Windows Vista (isiyo ingiliana na Windowa Me), Linux na Mac OS X

Sababu yenye uwezo mkubwa wa kusababisha kufeli ni video RAM ;programu hii imetengenezwa kuwaonya watumiaji ikiwa kadi yao ya grafiki haina uwezo wa kutosha wa kuendesha Google Earth (mara nyingi hii hutokea kutokana na video RAM zisizo na uwezo wa kutosha au programu za kuendesha kadi za grafiki zenye hitilafu). Jambo la pili lenye uwezo wa kusababisha kufeli ni kasi ya kufikia mtandao. Ila kwa wale wavumilivu sana, mtandao wa haraka wa Broadband (Cable, DSL, T1, nk) unahitajika.

Sifa bainishi za Linux

[hariri | hariri chanzo]
Mahitaji ya chini ya mfumo [27]
 • Kernel: 2.4 au ya baadaye
 • CPU: Pentium III, 500 MHz
 • Kikumbuko cha Mfumo(RAM): 128 MB
 • Diski: 400 MB nafasi
 • Kasi ya Mtandao: 128 Kbit / s
 • Kigao: 1024x768, rangi ya 16 bits
 • Imepimwa na inafanya kazi kwenye mifumo ifuatayo:
width = "50%" valign = "top" upana = "50%" valign = "top"

Kuvinjari kwenye Mtandao

[hariri | hariri chanzo]

Kufikia Google Earth 5, maelezo yaliyomo ya puto, ambayo yanaundwa katika KML kwa kutumia JavaScript na iFrame , yanatolewa yakiwa na injini iliyoundiwa ndani ya WebKit. [28]

Matoleo na tofauti zao

[hariri | hariri chanzo]

Muda wa matoleo

[hariri | hariri chanzo]
Inadhihirisha muda wa KML na historia ya Google Earth
 • Keyhole Earthviewer 1.0 - 11 Juni 2001
 • Keyhole Earthviewer 1.4-2002
 • Keyhole Earthviewer 1.6 - Februari 2003
 • Keyhole LT 1.7.1 - 26 Agosti 2003
 • Keyhole NV 1.7.2 - 16 Oktoba 2003
 • Keyhole 2.2 - 19 Agosti 2004
 • Google Earth 3.0 - 28 Juni 2005
 • Google Earth 4.0 - 11 Juni 2006
 • Google Earth 4.1 - 9 Mei 2007
 • Google Earth 4.2 - 23 Agosti 2007
 • Google Earth 4.3 - 15 Aprili 2008
 • Google Earth 5.0 - 5 Mei 2009
 • Google Earth 5,1 (beta) - 8 Septemba 2009
 • Google Earth 5.1 - 18 Novemba 2009

Toleo la Mac

[hariri | hariri chanzo]

Toleo la Mac OS X lilizinduliwa 10 Januari 2006, na linapatikana kwa kupakua kutoka kwenye tovuti ya Google Earth. Isipokuwa chache zilizotajwa hapo chini, toleo la Mac linaonekana kuwa imara na kamili, na lina huduma zote zinazopatikana kwenye toleo la Windows.

Viwambo na maelezo ya matekelezo halisi ya toleo la Mac yalifichuliwa kwenye Intanet tarehe 8 Desemba 2005. Toleo lililofichuliwa halikuwa kamilifu kwa kiasi kikubwa. Miongoni mwa udhaifu mwingine, menu ya Msaada wala kipengele cha "Leseni ya Kuonyesha" havikufanya kazi, kuonyesha kwamba toleo hili lilikusudiwa kwa matumizi ya ndani ya Google tu. Google haikutoa maelezo yoyote kuhusu tukio hili.

Toleo la Mac linaendeshwa tu chini ya toleo la Mac 10.4 OS X au ya baadaye. Hakuna kivinjari kilicho ndani, hakuna unganisho la moja kwa moja na Gmail na hakuna uchaguzi wa kuona kigao kizima. Kufikia Januari 2009 bado kulikuwa na hitilafu kadhaa kuhusu baa ya menu wakati unapobadilisha kati ya programu zinazotumiwa na pia hitilafu zinazohusu dokezo za bofu na uchapishaji.

Kutoka toleo 4.1.7076.4558 (lililozinduliwa tarehe 9 Mei 2007) kuendelea watumiaji wa Mac OS X wanaweza, miongoni mwa vipengele vingine vipya, kuboresha kwenda kwa toleo la "Plus" kupitia chaguo lililoko katika menu ya Google Earth. [29] Baadhi ya watumiaji waliripoti kutatizika Google Earth ilipopata hitilafu wakati walipokuwa wakitizama kwa karibu [30]

Toleo la Linux

[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia na toleo la 4 beta Google Earth linalofanya chini ya Linux, kama bandari ya asili kwa kutumia vifaa vya Qt. Ni programu yenye kipao mbele hasa ili kulazimisha Haki ya usimamizi wa dijitali; [onesha uthibitisho] Wakfu wa Programu za Bure unazingatia utengenezaji wa programu ya bure inayowiana na Google Earth kuwa mradi wenye umuhimu mkubwa wa programu za bure. [31]

Toleo la iPhone OS

[hariri | hariri chanzo]

Toleo la iPhone OS, ambalo linaendesha iPhone na iPod Touch, lilizinduliwa bila malipo kwenye hifadhi ya programu tarehe 27 Oktoba 2008. [32] {2/ Inatumia kusano ya kugusa mara nyingi kusonga juu ya tufe, kukaribisha au kuzungusha mandhari, na kuruhusu kuchagua mahali pa sasa kwa kutumia iPhone inayojumuisha GPS. Toleo hili, hata hivyo, halina kipengele cha safu kama matoleo ya kompyuta yalivyo. Kama Google Maps, inajumuisha tu safu za Panoramio na Wikipedia. [33]

Google Earth Plus

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kukomeshwa Desemba 2008, Google Earth Plus ilikuwa programu iliyounganishwa na Google Earth ambayo ilikuwa ikiwalenga watu binafsi waliojiandikisha kwa malipo na ilikuwa na vipengele ambavyo vingi sasa vinapatikana kwa Google Earth isiyo ya malipo:

 • Kuunganisha na GPS: kusoma ujumbe na alama za njia kutoka kifaa chaGPS. Aina mbalimbali ya programu zimetengezwa na makampuni mengine, programu hizi zinatoa huduma za kipengele hiki kwa kutumia toleo la kawaida la Google Earth kwa kutoa KML au faili za KML kwa kutegemea maelezo ya mtumizi au alama za njia zilizo rekodiwa na mtumizi. Hata hivyo, Google Earth Plus hutoa msaada wa moja kwa moja kwa bidhaa za Magellan na Garmin, ambazo kwa pamoja zinashikilia asilimia kubwa ya soko la GPS. Toleo la Linux la programu ya Google Earth Plus halitekelezi kama GPS.
 • Uchapishaji wa uangavu wa juu zaidi.
 • Msaada kupitia barua pepe.
 • Kiingiza data: soma pointi za anwani kutoka kwa faili za CSV; isiyozidi pointi / anwani 100. Kipengele kinachoruhusu kufasili njia na poligoni,ambayo inaweza kupelekwa kwa KML, kilikuwa awali kinapatikana kwa watumizi wa Plus pekee, lakini kiliwezeshwa kutumiwa bila malipo katika toleo la 4.0.2416.
 • Kasi ya juu ya kupakua data.

Google Earth Pro

[hariri | hariri chanzo]

Kwa kulipa ada ya $ 400 kwa mwaka, Google Earth Pro ni toleo la kibiashara na lina vipengele zaidi ya Google Earth na Google Earth Plus. Toleo la Pro lina programu zilizoongezwa kama:

 • Kutengeza filamu.
 • Kiingiza data ya GIS.
 • Moduli za uchapishaji za hali ya juu.

Mwanzoni vipengele hivi viligharimu zaidi mbali na ada ya $ 400, lakini hivi karibuni gharama hizo zimehusishwa kwenye malipo hayo.

Tofauti na toleo la Google Earth, toleo hili la kitaaluma halifanyi kazi na Linux.

Google Earth Enterprise

[hariri | hariri chanzo]

Google Earth Enterprise ni toleo la Google Earth lililoundwa kwa ajili ya matumizi ya mashirika ambayo biashara zao zingeweza kufaidika kutokana na utendakazi wa programu hiyo. [34]

Toleo la Portable

[hariri | hariri chanzo]

Toleo la Portable version la Google Earth, Archived 17 Machi 2009 at the Wayback Machine. lililotengenezwa na VMware ThinApp linapatikana. [35]. Toleo la portable version kwa ajili ya Linux Archived 8 Machi 2009 at the Wayback Machine. linapatikana pia, kwa kutumia mpangilio wa RUNZ.

Google Earth Plug-in

[hariri | hariri chanzo]

Google Earth API beta ni huduma isiyolipiwa , na unapatikana kwa mtandao wowote ambao unatumiwa na wateja bila malipo. Plug-in na JavaScript API yake huwezesha watumiaji kuweka toleo la Google Earth katika kurasa za mtandao. API haina vipengele vyote kamilifu vya programu ya Google Earth ,lakini inaruhusu kutengenezwa kwa programu za ramani za pande 3.

Google Earth Plug-in hivi sasa inapatikana kwa vivinjari mtandao na programu za mfumo zifuatazo:

Microsoft Windows (2000, XP, na Vista)

 • Google Chrome 1,0 +
 • Internet Explorer 6,0 +
 • Firefox 2,0 +
 • Flock 1.0 +

Apple Mac OS X 10.4 na zaidi (Intel na PowerPC)

 • Safari 3.1 +
 • Firefox 3.0 +

Hadi kufikia sasa plug-in inahudumia safu zifuatazo:

 • Mandhari
 • Barabara
 • Majengo
 • Mipaka
 • Majengo ya pande 3

Pia inawezesha 'Sky Mode', 'Photo Overlays', na hutoa kiasi sawa cha udhibiti na habari kama vile programu kamili.

Usahihi na uangavu

[hariri | hariri chanzo]
Faili:Google Scilly.jpg
Visiwa vidogo vya Scilly, kuonyesha uangavu wa chini sana wa baadhi ya visiwa. Visiwa (eneo la kijani ) ni zaidi ya kilomita 10 kwa upana. (Hii sasa imeboreshwa.) [64]


Faili:GoogleGib.jpg
Upande wa magharibi wa Gibraltar, mtazamo ulioinamishwa unaonyesha bahari ikipanda juu ya Mwamba wa Gibraltar - urefu wa bahari unaodaiwa katika ufukwe katika kumbukumbu za Elliot, ni mita 252 Hii sasa imerekebishwa. [65]

Maeneo mengi ya ardhi yamedhihirishwa katika picha za satelaiti zenye uangavu wa karibu 15 m kwa pixel. Picha hizi za msingi ni mita 30 zenye kuchukuliwa kwa masafa tofauti kwa kutumia programu ya Landsat ambayo ni programu ya kuunganisha picha zenye uangavu wa juu na zile zilizochukuliwa kwenye masafa tofauti au 'pansharpened' na picha zenye filamu nyeupe na nyeusi au ['panchromatic'] za Landsat za mita 15. Hata hivyo, Google inabadilisha picha hizi za msingi na picha za mita 2.5 za SPOTImage na seti data ya zingine zenye uangavu wa juu zilizotajwa chini. Baadhi ya vituo vya idadi kubwa ya watu pia vimedhihirishwa na picha za ndege yaani (orthophotography) na pixels kadhaa kwa mita. Bahari zinadhihirishwa kwa uangavu wa chini, kama ilivyo na baadhi ya visiwa; hasa, visiwa vya Scilly vilivyo Kusini Mashariki mwa Uingereza, vilikuwa kwenye uangavu wa mita 500 au chini, hata hivyo jambo hilo sasa limetatuliwa.

Google imerekebisha ukosefu wa uhakika kwenye vekta ya kuweka ramani tangu kuzinduliwa kwa programu, bila kuhitaji kurekebisha programu yenyewe. Mfano wa jambo hili ni kukosekana kwa mipaka ya ramani ya eneo la Nunavut nchini Canada kwa Google Earth, ni wilaya ambayo ilikuwa imeundwa tarehe 1 Aprili 1999; kosa hili lilirekebishwa na mojawapo ya marekebisho ya data, mapema mwaka 2006. Nyongeza za hivi karibuni ziwezesha picha zenye habari za kina, hasa katika maeneo fulani ya Ulaya Magharibi na Kati.

Picha hazipigwi kwa wakati mmoja, lakini zote zimepigwa katika kipindi kisichozidi miaka mitatu. Hata hivyo baada ya kuzinduliwa kwa Google Earth 5.0, ina picha za kihistoria za hadi miaka ya 1940 katika maeneo mengine. Seti za picha mara nyingine hazijaunganishwa vizuri. Nyongeza kwa hifadhi data ya picha inaweza kuonekana mara moja moja hasa wakati mabadiliko makubwa yanapoonekana kwenye mandhari, kwa mfano nyongeza zisizokamilika za Google Earth za New Orleans kuhusu kimbunga cha Katrina kilichotokea, au wakati alama za mahali zinaonekana kuhama bila kutarajiwa kwenye uso wa Dunia. Ingawa bado alama za mahali hazijasonga, picha zinatengezwa na kuunganishwa kwa njia tofauti tofauti. Nyongeza kama hizi kwa picha za London mapema 2006 zilisababisha kuhama kwa karibu mita 15-20 katika maeneo mengi, jambo lililoonekana kwa sababu uangavu ni wa juu sana.

Majina ya mahali na kina cha habari hutofautiana sana kutoka mahali pamoja hadi pengine. Ni sahihi zaidi katika Amerika ya Kaskazini na Ulaya, lakini kurekebisha kwa mara kwa mara kwa ramani kunaimarisha hali ya kufikiwa kwa sehemu zingine.


Makosa wakati mwingine hutokea kutokana na teknolojia iliyotumika kupima urefu wa Mandhari; kwa mfano, majengo marefu katika Adelaide, Australia kusababisha sehemu moja ya mji kuonyeshwa kama mlima mdogo, wakati ukweli ni kuwa ni mahali tambarare. Urefu wa Eiffel Tower unasababisha athari kama hiyo katika uonyeshaji wa Paris. Pia, kabla ya kuzinduliwa kwa toleo 5.0 Februari 2009, mwinuko chini ya usawa wa bahari uliwasilishwa kama usawa wa bahari, kwa mfano: Mji wa Salton, California; Death Valley; na Dead Sea zote zilionyeshwa kama mita 0 wakati Mji wa Salton ni -38 ; Dead Valley ni mita -86; na Dead Sea ni mita -420.

Wakati hakuna data ya kimo ya dijitali ya sekunde tao 3 [[]] si picha zote za pande tatu zinazofunika sehemu za miinuko ni sahihi, lakini sehemu nyingi za milima sasa zimebainishwa vizuri. Mfumo wa msingi wa muinuko wa dijitali umewekwa sekunde tao 3 mbali mno kaskazini na hadi sekunde tao 3 mbali mno magharibi. Hii ina maana kuwa baadhi ya matiko ya mlima yanaonekana kimakosa kuwa na vivuli kuenda pande zake za kusini. Baadhi ya picha za uangavu wa juu zimewekwa kimakosa, mfano ni picha ya Annapurna, ambayo imewekwa kimakosa kwa karibu sekunde tao 12. Data ya mwinuko hivi karibuni ilisasishwa hadi uangavu wa mita 10(sekunde tao 1/3) katika maeneo mengi ya Amerika kutoka ile ya awali ya mita 30(sekunde tao 1).

Kipengele cha kupima kinaonyesha kwamba urefu wa ikweta ni karibu kilomita 40,030.24, inakosea kwa aslimia -0.112 ikilinganishwa na kipimo halisi cha kilomita 40,075.02 duniani; kwa mduara wa meridian, inaonyesha urefu wa juu wa kilomita 39,963.13, pia inakosea kwa asilimia -0.112 ikilinganishwa na thamani halisi ya kilomita 40,007.86.


Mnamo 16 Desemba 2007, sehemu kubwa ya Antaktika ilirekebishwa kufikia uangavu wa mita 15 kwa kutumia picha kutoka Landsat Image Mosaic ya Australia; (Picha za uangavu wa mita 1 za Antarctica ziliongezwa Juni 2007); hata hivyo, ncha ya barafu ya Arctic, haimo kabisa katika toleo la sasa la Google Earth, kama vile mawimbi ya bahari. Ncha ya kaskazini ya kijiografia hupatikana ikielea juu ya Bahari ya Arctic, mfumo wa kutengeza tofali unatoa vitu vilivyobuniwa /0} karibu na ncha huku tofali zikiwa ndogo zaidi na makosa ya kutokana na kupeleka kwenye mfumo wa juu kulimbikizwa.

Kufunikwa na mawingu kunaweza kufanya sehemu za ardhi zisiweze kuonekana au zisionekane vizuri, zikiwemo sehemu za kivuli cha milima .

Ubishi /ukosoaji

[hariri | hariri chanzo]

Programu imekosolewa na makundi yenye maslahi maalumu, ikiwa ni pamoja na viongozi wa kitaifa, kama kuwa ni uvamizi wa faragha na hata kuwa tishio kwa usalama wa taifa. Hoja ya kawaida inayotolewa ni kuwa programu inatoa habari kuhusu vyombo vya kijeshi au vifaa vingine muhimu amabvyo vinaweza kutumiwa na magaidi s. Yafuatayo ni baadhi ya maswala yanayoleta ubishi:

 • Aliyekuwa rais wa India APJ Abdul Kalam ameelezea wasiwasi wake juu ya upatikanaji wa picha za uangavu wa juu za maeneo nyeti nchini India. [36] Google hatimaye ilikubali kuziwekea vikwazo tovuti hizo. [37]
 • Shirika la India la Utafiti wa Anga limesema Google Earth inaleta tishio kwa usalama wa India na linaomba kuzungumzia jambo hili na maafisa wa Google. [38]
 • Google imeweka ishara nyekundu kwenye maeneo yote ya mpaka wa Kaskazini kuonyesha ugomvi juu ya maeneo ya Kashmir.
 • Serikali ya Korea Kusini imeelezea wasiwasi kwamba programu inatoa picha ya ikulu na maeneo ya kijeshi hali inayoweza kutumiwa na adui wao jirani Korea ya Kaskazini. [39]
 • Katika mwaka 2006, mtumiaji mmoja aliona maelezo ya mandhari ya sehemu kubwa katika eneo la mashambani nchini Uchina. Kielelezo hicho ni toleo la skeli ndogo (1 / 500)ya Milima ya Karakoram ,ambayo sasa iko chini ya utawala wa Uchina lakini inayodaiwa na India. Baadaye ilipothibitishwa kuwa kielelezo hicho kilikuwa cha eneo hilo, watazamaji walianza kuhofia shambulizi la kijeshi. [40] [41]
 • Mtoaji mkuu wa huduma za mtandao nchini Morocco, kampuni ya Maroc Telecom imekuwa ikizuia Google Earth [42] tangu Agosti 2006 kwa sababu zisizojulikana.
 • Wasimamizi wa kiwanda cha Kinyuklia cha Lucas Heights huko Sydney, mkoa wa New South Wales, Australia waliiomba Google isionyeshe picha za uangavu wa juu za kiwanda hicho. [43] Hata hivyo, baadaye waliondolea mbali ombi hilo. [44]
 • Mnamo Julai 2007, iliripotiwa kuwa manowari mpya ya Kichina ya jeshi la majini ya Jin-class ya makombora ya kinyuklia ilipigwa picha katika kituo cha Manowari cha Xiaopingdao kusini mwa Dalian. [45]
 • Hamas na kundi la kujitolea mhanga la al-Aqsa Brigade limeripotiwa kutumia Google Earth kupanga mashambulizi ya roketi aina ya Qassam hadi Israel kutoka Gaza (Angalia: Orodha ya mashambulizi ya roketi za Qassam.) [46] [47]
 • Mshambulizi wa pekee wa bunduki katika mashambulizi ya Mumbai ya 2008 alikiri walitumia Google Earth ili kujifahamisha na maeneo ya mashambulizi. [48]
Faili:Royal Stables.jpg
Picha isiyoonekana vizuri ya Royal Stables mjini Hague, Uholanzi.

Baadhi ya wananchi wanaweza kuelezea wasiwasi wao kuhusu usambazaji wa habari ya angani inayoonyesha mali na makazi yao kuwa bila vikwazo. Kwa vile kuna sheria chache za kumhakikishia mtu haki ya faragha, kinyume na haki ya usiri kwa taifa, hili ni jambo linalobadilika lakini lisilo na umuhimu mkubwa. Labda kwa kufahamu shutuma hizi[49] kwa muda, Google iliweka eneo la 51 (ambalo linaonekana na kupatikana kwa urahisi) katika Nevada kama mahali pa kwanza kuonekana wakati Google Earth inapowekwa.

Kutokana na shinikizo kutoka serikali ya Marekani, makazi ya Makamu wa Rais yaliyo Number one Observatory Circle yalifunikwa kwa kutumia piseli chache katika Google Earth na Google Maps, lakini jambo hili limeondolewa kwa sasa. Umuhimu wa kufunikwa huku ulikuwa hauna maana kwani, picha za uangavu wa juu, na za ukaguzi wa angani za makao hayo zinapatikana kwenye tovuti zingine katika mtandao. [50] Capitol Hill pia ilikuwa ikionyeshwa kwa piseli chache lakini kikwazo hiki sasa kimeondolewa.

Wakosoaji wameelezea wasiwasi juu ya utayari wa Google kulemaza seti ya data yao ili kukidhi matakwa maalum, ikiamini kuwa kuziba sehemu yoyote kimakusudi inaenda kinyume na lengo lao kuu la kumfanya mtumiaji "kuashiria kwa kivinjari na kukaribia mahali popote kwenye duniani unapotaka kupachunguza". [51]

Matoleo ya majuzi ya Google Earth yanahitaji programu inayoendeshwa kwa nyuma ambayo itapakua na kupokea marekebisho mapya kwenye picha moja kwa moja. Watumiaji wengi walieelezea wasiwasi wao kwani hakuna njia rahisi ya kuisimamisha programu hii. [52]

Hakinakili

[hariri | hariri chanzo]

Kwa sasa picha zote zinazotengezwa na Google Earth kutokana na data za satelaiti za Google Earth ni ramani zilizowekewa hakinakili. Kazi yoyote inayotokana na data iliyowekewa hakinakili na Google, katika Sheria ya hakinakilikili ya Marekani, haiwezi kutumika ila chini ya leseni iliyotolewa na Google. Google inaruhusu matumizi ya picha ya kibinafsi yasiyo ya kibiashara (mfano kwenye tovuti ya kibinafsi au blogu) bora tu hakinakili na umiliki uhifadhiwe. [53] Tofauti ni kwamba, picha za programu ya NASA ya World Wind hutumia Blue Marble, Landsat au safu ya USGS, kila moja ni safu ya Mandhari inayoweza kuonekana kwa kila mtu. Kazi yoyote iliyofanywa na shirika la serikali ya Marekani inaruhusiwa kuonekana kwa kila mtu punde tu inapokamilika. Hii ina maana kwamba picha zile zinaweza kurekebishwa bila pingamizi , kusambazwa na kutumiwa kwa madhumuni ya kibiashara bila kikwazo. najaribu kuweka marekebisho katika ukurasa huu kwa sababu yapo makosa ya tafsiri ya neno Hakimiliki na Hakinakili na kwa ufasaha zaidi unapozungumzia ne la kiingereza la Copyright una maanisha Haki/Nakili yapo makosa ambayo siku zote yamekuwa yakifanywa na wanasiasa kwa kupotosha maana ya neno hili. ukweli ni kwamba mtu anaweza akamiliki kazi ya mtu lakini asiwe na uwezo wa kumfanya mwingine ainakili ndiyo maana tunasema Hakimiliki na Hakinakili ni mambo mawili tofauti. embu fikiria maneno yenyewe ni haya, yaangalie ukianza na kiingereza (copy na right) neno ("Copy" maana yake Nakili. lakini pia "Right" maana yake Haki) unapochanganya na neno Miliki ni juu ya mtu kupewa haki ya kudurufu na kwa maana ya kuimiliki kwa wakati huo ambapo pia muda huo wa umiliki hufika kikomo na bado haki ya kunakili ikabaki mikononi mwa mwenye hakinakili.

Google Earth pia inajumuisha safu kama chemichemi ya habari kuhusu biashara na sehemu zingine za manufaa, vilevile kuonyesha habari ya jamii nyingi, kama vile Wikipedia, Panoramio na YouTube. Google huongeza habari mpya kupitia safu mara kwa mara. Safu nyingi za Google Earth, kama vile Panoramio na Google Earth Community zinaongezewa habari kila siku kutoka kwa tovuti husika.

Mtandao wa Kijiografia

[hariri | hariri chanzo]
 • Panoramio: Inaonyesha picha nyingi zenye umaana zilizopakiwa kwenye tovuti ya Panoramio
 • Wikipedia: Inaonyesha muhtasari wa makala ya Wikipedia, mara nyingi juu ya mahali au matukio
 • Mahali
  • Mahali: muhtasari kuhusu maeneo muhimu ulimwenguni. Baadhi ya alama za mahali zimechukuliwa kutoka makala yanayotoka kwa Google Earth Community na baadhi ya makala ya Wikipedia. [54]
  • Utangulizi: Unaonyesha muhtasari wa yaliyomo kwenye baadhi ya safu. Ikiwa safu mpya imeongezwa, safu ya utangulizi itaanzishwa kama ya kwanza wakati programu itakapoendeshwa tena.

Barabara

[hariri | hariri chanzo]

Inaonyesha barabara zilizopo. Rangi na ishara zinazoonyeshwa zinatofautiana kutegemea aina ya barabara.

Majengo ya Pande 3

[hariri | hariri chanzo]

Inaonyesha majengo mengi kwa pande tatu katika miji mikubwa kama New York au Hong Kong, katika mitindo ifuatayo:

 • Picha za kihalisia: Inaonyesha majengo mengi katika mtindo wa kuaminika, ikiwa na poligoni na picha za sura.
 • Kijivu: {0Picha za majengo yaliyojengewa kompyuta ambazo hazionyeshi sifa nyingi } na hazina uwezo wa kuonyesha vipengele kama vya picha za kihalisia.

Google Street View

[hariri | hariri chanzo]

Inaonyesha ishara za mahali kwa mtazamo wa digrii 360 wa panoramic ya mitaa ya miji mingi nchini Australia, Ufaransa, Italy, Ujapani, New Zealand, Uhispania, Marekani, na hivi karibuni Ureno, Uingereza, Uholanzi, Taiwan, Uswidi, Uswisi na Canada.

Mipaka na Kitambulisho

[hariri | hariri chanzo]

Ina mipaka ya nchi / mikoa na huonyesha alama za mahali za miji na miji mikuu.

 • Mipaka: Inaashiria mipaka ya kimataifa kwa kutumia msitari mnene wa manjano, mipaka ya ngazi 1 ya kiutawala (kwa ujumla majimbo na mikoa) kwa laini ya rangi ya Lavenda, na mipaka ya utawala ya ngazi ya 2 (mataifa) na laini ya rangi ya sian. Fuo za bahari zinabainishwa kwa laini nyembamba za manjano. Inaonyesha majina ya nchi, maeneo ya ngazi ya 1 ya utawala, na visiwa.
 • Sehemu zenye wakazi: Inaonyesha majina ya miji mikuu, miji, vijiji, maeneo teule ya sensa (CDPs), na vitongoji.
 • Majina mbadala ya Mahali: Nyingi ya miji mikuu katika nchi zisizo za Kiingereza zilipewa majina katika lugha zao za kiasili ili kuepuka haja ya ujanibishaji mkubwa Safu hii inaonyesha majina kama haya katika Kiingereza.
 • Kitambulisho: Kinaonyesha majina ya mikusanyiko mikubwa ya maji, kama vile bahari, na mito ya bahari.

Mwendo wa magari barabarani

[hariri | hariri chanzo]

Inaonyesha viashiria vya rangi kwenye barabara ambapo hali ya mwendo wa magari barabarani unapimwa. Viashiria vya kijani hutumiwa kwa hali ya mwendo wa magari isiyokuwa nzuri , manjano kwa kasi ya chini, na nyekundu kwa hali mbaya ya mwendo wa magari. Kwa kubonyeza kiashiria, mtumiaji anaweza kuona jina la barabara na kasi ya magari katika barabara hiyo. Haijulikani viashiria hivi husasishwa mara ngapi.

Hali ya anga

[hariri | hariri chanzo]
 • Mawingu - Inaonyesha mfuniko wa mawingu kwa kutegemea data kutoka kwa satelaiti zilizo mahali pamoja na zile zinazoizunguka dunia. Mawingu huonekana katika mwinuko uliokadiriwa, kuamuliwa kwa kupima joto la juu la mawingu likilinganishwa na joto la juu la ardhini. [55]
 • Rada - Inaonyesha hali ya hewa ya rada kutokana na data inayotolewa na weather.com na Shirika la Hali ya Anga ya Kimataifa, zinazotoa habari mpya kila dakika 5-6. [55]
 • Hali na Kutabiri- Inaonyesha joto la mahali na hali ya anga. Kubonyeza kiashiria kunaonyesha hali ya anga kamili ya mahali ulipo, inatolewa na weather.com. [55]
 • Habari- Wakibonyeza habari watumaji wanaruhusiwa kusoma zaidi juu ya pale ambapo Google Earth inapata habari ya hali ya hewa. [55]

Hifadhi ya picha

[hariri | hariri chanzo]
 • Roma ya zamani: Ilizinduliwa na Google tarehe 12 Novemba 2008
 • Discovery Networks: Inaonyesha habari za kijiografia kutoka kituo cha televisheni cha Discovery Channel.
 • {0European Space Agency:{/0} Inaonyesha picha nyingi za satelaiti zilizopigwa za Dunia.
 • Gigapan photos: Picha kutoka mradi wa Google wa Gigapan .
 • GigapxlPhotos: Picha zilizopigwa kutumia Gigapxl.
 • Google Book Search: matumizi ya kipengele cha kutafuta vitabu cha Google katika Google Earth.
 • Google Eart Community: Onyesho la faili zote za viingilio katika Jamii ya Google Earth.
 • { Google News:{/0} Inaonyesha habari kutoka chemichemi nyingi za habari ulimwenguni .
 • NASA: Onyesho la picha nyingi za satelaiti, sehemu za ramani zilizoshikamana na habari kutoka NASA.
 • National Geographic Magazine: Inaonyesha habari zilizomo katika jarida la National Geographic Magazine. .
 • New York Times: ukusanyaji wa taarifa za habari kutoka gazeti maarufu la New York Times.
 • Rumsey Historical Maps: Inaonyesha mkusanyiko wa ramani za kihistoria, za miaka ya nyuma kufikia miaka ya 1600.
 • Usafiri na Utalii
 • Trimble Outdoor Trips: Mkusanyiko wa njia za kutalii zilizorekodiwa.
 • Volkeno
 • Webcams travel: Ni mkusanyako wa kamera za Webcam kote duniani/0}
 • YouTube: Mkusanyiko wa video maarufu zilizoko katika tovuti ya YouTube.

Uelewa wa Duniani

[hariri | hariri chanzo]

Mkusanyiko wa huduma za kueneza uelewa wa Dunia nzima. Safu hii ilitolewa na Google Earth Outreach.

Mahali pa kuvutia

[hariri | hariri chanzo]

Mkusanyiko wa sehemu za kibiashara unaotolewa na huduma nyingi za mitaa.

Safu za Angani

[hariri | hariri chanzo]

Safu za Google Sky.

Safu za Mirihi

[hariri | hariri chanzo]
 • Picha za Satelaiti
 • Majina ya Mahali
 • Ramani za Dunia
 • Picha za vyombo vya angani
 • Picha za Mirihi
  • Wanaosafiri na kutua huko.
  • Mwongozo wa Msafiri kwa Mirihi

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Watoa Picha

[hariri | hariri chanzo]
 1. "Google Earth Plus Discontinued".
 2. "Google Discontinues "Google Earth Plus"".
 3. "Google Earth Product Family". Iliwekwa mnamo 2007-08-05.
 4. "Google Earth, meet the browser".
 5. "Media Coverage of Geospatial Platforms". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-26. Iliwekwa mnamo 2007-08-05.
 6. Google Earth Coverage: Ramani zinazoonyesha uwakilishi wa maelezo ya Google Earth
 7. "Google Earth Community: Nov. 23rd - Thanksgiving Day imagery update". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-18. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.
 8. "Bohari ya pande 3 (3D)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-02-24. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.
 9. http://www.gearthblog.com/blog/archives/2009/01/new_view_of_ocean_floor_in_google_e.html
 10. "Google is planning to acquire Panoramio". google.com.
 11. [22] ^ Blogu ya Marco: Kiigiza kuruka angani cha Google Earth
 12. "Explore the sky with Google Earth". Google. 2007-08-22. Iliwekwa mnamo 2007-08-22.
 13. [28] ^ Badiri za kuongezwa katika Google Earth ishara katika Stars- Tech - 22 Agosti, 2007 - New Scientist Tech Archived 11 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
 14. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-18. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.
 15. http://news.bbc.co.uk/1/hi/technology/7865407.stm
 16. "Google Earth now includes US "Third Coast"".
 17. "Dive into New Google Earth". Iliwekwa mnamo 2009-02-03.
 18. http://www.gearthblog.com/blog/archives/2009/07/look_at_the_moon_in_google_earth_-.html
 19. http://www.gearthblog.com/blog/archives/2009/07/google_earth_event_on_july_20th_in.html
 20. http://google-latlong.blogspot.com/2009/07/fly-yourself-to-moon.html
 21. [41]Web User-Google Earth interview.
 22. [42] ^ Avi Bar-Ze'ev (kutoka Keyhole, mtangulizi wa Google Earth) juu ya asili ya Google Earth Archived 12 Oktoba 2008 at the Wayback Machine.
 23. [43] ^ Google Earth: Kutoka angani hadi usoni mwako.... na zaidi
 24. [44] ^ Ripoti ya hakika isiyo na mwisho Archived 11 Januari 2016 at the Wayback Machine.
 25. [45] ^ Dondoo za ufunguzi wa Google Earth / Logi ya Historia ya mabadiliko
 26. Google Earth
 27. "Google Earth". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-11. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.
 28. Maandiko ya Marejeo ya KML - <maelezo>
 29. "Google Earth 4.2.180.1134 - MacUpdate". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-10-15. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.
 30. "Google Earth Community: Viewing forum: Google Earth for Mac OS X". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-17. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.
 31. [54] ^ [1] FSF: Miradi ya programu zisizo za malipo zenye umuhimu mkubwa.
 32. Sorrel, Charlie (2008-10-27). "Google Earth Comes to the iPhone". Wired. Iliwekwa mnamo 2008-10-27. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
 33. http://www.gearthblog.com/blog/archives/2008/10/google_earth_for_the_iphone_release.html
 34. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-27. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.
 35. [62] ^ Programu rahisi kuhamisha zaPortable Application (Windows) Archived 17 Machi 2009 at the Wayback Machine.
 36. "Kalam Concerned Over Google Earth". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-01-02. Iliwekwa mnamo 2007-01-25.
 37. ""Google Earth agrees to blur pix of key Indian sites"".
 38. ""Google Earth Poses Security Threat to India, ISRO Chief seeks Dialogue"". Iliwekwa mnamo 2007-01-25.
 39. ""Google Earth images compromise secret installations in S. Korea"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-07-01. Iliwekwa mnamo 2007-01-25.
 40. ""Chinese X-file excites spotters"". Iliwekwa mnamo 2007-01-25.
 41. ""From sky, see how China builds model of Indian border 2400 km away"". Iliwekwa mnamo 2007-01-25.
 42. [78] ^ Ujumbe kwa ulimwengu
 43. ""Google Earth prompts security fears"". Iliwekwa mnamo 2007-01-25.
 44. "" Aussie Nuclear Reactor on Google Earth"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-10-17. Iliwekwa mnamo 2007-01-25.
 45. ""New Chinese Ballistic Missile Submarine Spotted"". Iliwekwa mnamo 2007-07-10.
 46. [85] ^ Google Earth inatumika kulenga Israeli
 47. Hutcheon, Stephen. "We're not stalking you or helping terrorists, says Google Earth boss", Sydney Morning Herald, 2009-01-30. Retrieved on 2009-11-07. Archived from the original on 2009-02-03. 
 48. [88] ^ "mashambulizi ya Mumbai: India ilianzisha kesi dhidi ya Google Earth juu ya matumizi picha na magaidi", The Daily Telegraph, 9 Desemba 2008.
 49. [89] ^ Kesi ya faragha dhidi Google Earth, Blogu ya Sheria ya Angani, 09/04/2008
 50. "Eyeballing the US Vice Presidential Residence".
 51. ""The Creative Reconstruction of the Internet: Google and the Privatization of Cyberspace and DigiPlace"" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-05-17. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.
 52. ""Why Google's Software Update Tool Is Evil"".
 53. [96] ^ Eneo la Msaada la Google Earth: Naweza pakia picha kwa mtandao?
 54. http://www.gearthblog.com/blog/archives/2008/08/august_geographic_web_layer_update.html
 55. 55.0 55.1 55.2 55.3 [98] ^ Google Earth: Safu ya hali ya hewa, habari zilizounganishwa - zilizotizamwa: 3 Machi 2009 v5.0.11337.1968 (beta)
 56. "Google Earth / SketchUp na Oracle Spatial". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-09. Iliwekwa mnamo 2009-12-02.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Tovuti Rasmi na zinazohusiana

[hariri | hariri chanzo]

Miongozo na vidokezo visvyo rasmi

[hariri | hariri chanzo]

Alama za mahali na ishara zilizoshikama kwenye ramani

[hariri | hariri chanzo]
 • GeoServer Archived 2 Machi 2008 at the Wayback Machine. - Seva ya kuzalisha faili za KML kutoka Shapefiles, ArcSDE, Oracle, PostGIS, MySQL, GeoTiff, ArcGrid, pamoja na msaada kwa viungo vya Mtandao, ishara kubwa zilizoshikamana kwenye ramani, vitokeo vya muda kwa muda.
 • GPSVisualizer - kubadili data ya GPS kwa matumizi ya Google Earth.
 • Google Earth Toolbox - Matlab & Octave zinashughulika kutoa faili za KML.
 • geolyzer - maabara yanayotegemea programu ya kuchunguza urahisi wa utumizi kwa Google Earth.