Blogu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Blogu ni teknolojia mpya inayowezesha watu binafsi kuchapa maoni na fikra zao katika mtandao wa tarakilishi. Blogu inaweza kuchukuliwa kama ni shajara pepe.

Neno la Kiswahili "blogu" linatokana na neno la Kiingereza, "blog", ambalo limetokana na neno lingine, "weblog".

Kimsingi, blogu ni aina ya tovuti ambayo huandikwa mara kwa mara na kwa mpangilio wa mambo mapya kutokea ukurasa wa mbele kuendana na tarehe na mwezi.

Zipo blogu za aina mbalimbali. Kwa mfano, blogu za maandishi, blogu za mkononi, blogu za picha, blogu za sauti, na blogu za video.

Blogu ya mradi wa Global Voices inaandika muhtasari wa majadiliano na habari zinazojitokeza katika blogu mbalimbali duniani, hasa nje ya Marekani. Mradi huu una wanablogu katika nchi mbalimbali duniani ambao wanaandika juu ya masuala muhimu yanayojitokeza katika blogu za nchini mwao au katika bara lao.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Blogger Templates[hariri | hariri chanzo]