Google

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Google
Aina ya shirika Public
Alama Kigezo:NASDAQ
Kigezo:NASDAQ
NASDAQ-100 Component
S&P 500 Component
Tarehe ya kwanza Menlo Park, California
(Septemba 4, 1998 (1998-09-04))[1][2]
Mwanzilishi Sergey Brin, Larry Page
Pahali pa makao makuu , Mountain View, California, U.S.[3]
Pahali pa wateja Worldwide
Watu muhimu
Sekta ya viwanda Internet
Computer software
Telecoms equipment
Bidhaa See list of Google products
Mapato increase US$ 59.82 billion (2013)[4]
Mapato kasoro ushuru increase US$ 13.96 billion (2013)[4]
Faida increase US$ 12.92 billion (2013)[4]
Jumla ya mali increase US$ 110.92 billion (2013)[4]
Thamani increase US$ 87.30 billion (2013)[4]
Wafanyakazi 49,829 (Q1 2014)[5]
Tovuti google.com

Google ni tovuti kwenye mtandao inayotumika kutafuta kurasa na habari za kila aina. Inatumia programu inayoitwa "mashine ya kutafuta" (search engine). Jina Google limetokana na neno Googol linalomaanisha tarakimu 1 inayofuatwa na sifuri 100.

Imepata mafanikio makubwa kati ya tovuti za aina hii, na kila siku takriban watu milioni 200,000 wanaitumia.[6]

Tovuti ni mali ya kampuni Google Inc. ya Marekani, lakini kampuni mama ni Alphabet Inc.. Kampuni ilianzishwa na Larry Page and Sergey Brin mwaka 1998, wakati walipokuwa wanafunzi wa chuo kikuu.

Matumizi ya Google ni bure, lakini kampuni ina mapato makubwa kutokana na matangazo ya biashara kwenye kurasa zake na thamani ya kampuni imekadiriwa kuwa bilioni za dolar 130 hivi.[7] Umaarufu wa mashine ya kutafuta ya Google umetokana na sababu mbalimbali ikiwemo kanuni zinazotumika kuzipa ukurasa daraja la mtandaoni kwa kutumia mfumo uliopewa jina la PageRank kutokana na jina la mmoja wa waanzilishi wa Google, Larry Page.[8] watangazaji wengi hujitahidi kutumia mbinu mbalimbali ili kuwa na daraja la juu kwenye mashine yake ya kutafuta.[9]

Kiasili Google ilitengenezwa kwa kutafuta maneno kwenye tovuti na hadi leo hii matumizi yake ni makubwa. Lakini Google imeendelea kuongeza huduma nyingine kama kutafuta picha (Google Images), kutafuta mahali kwenye ramani ya dunia (Google Maps), kutafuta habari kwenye wavuti ya magazeti (Google News), video (YouTube) na mengine mengi.

Nje ya huduma za kutafuta, google imeanzisha pia huduma nyingine kama 'Google Mail' (huduma ya barua pepe) au huduma za kutunza kalenda (Google Calendar) na maandishi ya binafsi ya akaunti kwenye seva za google.

Huduma nyingine ni ile ya kutafsiri (Google Translate) yenye nafasi ya kupakia matini kutoka moja ya lugha 60 na programu inajaribu kuitafsiri kwa lugha nyingine. Kati ya lugha kubwa kama Kiingereza, Kihispania au Kifaransa matokeo ni mazuri kiasi, lakini lugha ndogo kama Kiswahili bado hayajaridhisha ingawa inaendelea kuboreka polepole.

Kuna pia jaribio la kutoa google kwa lugha ya Kiswahili lakini hii inaleta tu ukurasa wa kuingia katika tovuti iliyotafsiriwa kisehemu.[10].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Company. Google. Iliwekwa mnamo August 31, 2011.
  2. Claburn, Thomas. Google Founded By Sergey Brin, Larry Page... And Hubert Chang?!?. InformationWeek. Iliwekwa mnamo August 31, 2011.
  3. Locations - Google Jobs. Google.com. Iliwekwa mnamo 2013-09-27.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 Google Inc, Form 10-K, Annual Report, Filing Date Jan 29, 2013. secdatabase.com. Iliwekwa mnamo Mar 8, 2013.
  5. Google's Income Statement Information. Google.
  6. Taarifa ya searchenginewatch Aprili 2011
  7. taarifa ya kampuni ya Millwardbrown ya mwaka 2010
  8. Google Press Center: Fun Facts. www.google.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2001-07-15.
  9. "Google Ranking.
  10. http://www.google.com/ig?hl=sw

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]