Nenda kwa yaliyomo

Kyoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kituo cha reli Kyoto.
Hekalu ya Shinto mjini Kyoto.
Kyoto, 1891

Kyoto ni mji wa Japani uliokuwa mji mkuu wa nchi kati ya 794 na 1868. Ilikuwa makao makuu ya Tenno (Kaisari) wa taifa. Iko takriban kilomita 400 kusini magharibi ya Tokyo kwenye kisiwa cha Honshu.

Sasa Kyoto ni mji mkubwa wa tatu nchini iliwa na wakazi milioni moja na nusu. Ni makao makuu ya mkoa wa Kyoto. Kuna taasisi za utamaduni na elimu pamoja vyuo vikuu.

Kyoto ni kati ya miji ya kale ya Japani. Kuna majengo mengi ya kihistoria kama mahekalu, majumba ya matenno na nyumba za kidesturi. Majengo kadhaa yameigizwa na UNESCO katika orodha ya urithi wa dunia.

Mazingira ya Kyoto pana milima mingi. Imepoteza cheo cha mji mkuu wakati Tenno Meiji alipohamisha makao yake kutoka hapa kwenda boma la Edo iliyokuwa Tokya baadaye.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Japani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kyoto kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: