Nenda kwa yaliyomo

Melbourne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Yarra mjini Melbourne

Melbourne ni mji mkubwa katika Australia ya kusini na mji mkuu wa jimbo la Victoria. Ina wakazi 3,720,300.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mji uliundwa mwaka 1835 kando ya hori ya Port Phillip Bay ya Pasifiki. Ilikua haraka baada ya kupatikana dhahabu tangu mwaka 1851. Imekuwa kitovu cha uchumi, utamaduni na michezo. Katika karne ya 19 ilikuwa mji mkubwa wa Australia na pia mji mkuu wa taifa hadi uhamisho wa bunge kwenda Canberra mwaka 1901.

Siku hizi kuna wakazi kutoka nchi nyingi waliohamia Australia na kukaa mjini. Robo ya wakazi wake walizaliwa nje: kuna watu kutoka nchi 233 na lugha 180 zinajadiliwa mjini hata kama theluthi mbili za wakazi hutumia Kiingereza kwao nyumbani.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Melbourne kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.