Nenda kwa yaliyomo

Canberra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Canberra

Mhimili wa Bunge mjini Canberra kati ya jengo la bunge na makumbusho kwa marehemu wa vita kuu
Habari za kimsingi
Utawala Australian Capital Territory
Historia iliundwa 12 Machi 1913 na kuwa mji mkuu 9 Mei 1927
Anwani ya kijiografia Latitudo: 35°18'30"S
Longitudo: 149°7'30"E
Kimo 632 m juu ya UB
Eneo 805.6 km²
Wakazi 332,798 (2006)
Msongamano wa watu watu 401 kwa km²
Simu +56 (nchi) 73 (mji)
Mahali

Canberra ni mji mkuu wa Australia mwenye wakazi 330,000. Si sehemu ya jimbo lolote la shirikisho la Australia lakini limepewa eneo lake la kitaifa kando la mto Molonglo ndani ya eneo la jimbo New South Wales.

Ramani ya Canberra

Iko kilomita 300 kusini magharibi ya Sydney na kilomita 650 kaskazini-masahriki ya Melbourne.

Mji wa kupangwa

[hariri | hariri chanzo]

Canberra ni mji mpya uliopangwa na ujenzi ukaanza mwaka 1913. Msanifu Mwamerika Walter Burley Griffin alipanga ramani ya mji mwenye bustani nyingi na barabara zilizufuata mpangilio wa duara, pembetatu na miraba.

Alianza kwa kuchukua mto Molongolo kama mhimili wa maji unaokatwa na mhimili wa kwanza kwenye nchi ni uwazi kati ya nyumba ya bunge na makumbusho kwa ajili ya marehemu wa vita.

Mistari mingine muhimu ni "pembetatu ya bunge" kwa barabara tatu pana na nyofu kati ya kilima cha bunge, kilima penye kitovu cha mji mwenyewe na kilima penye wizara ya jeshi. Mikono miwili ya pembetatu inayotoka bungeni inavuka mto kwa madaraja.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuundwa kwa Canberra miji ya Sydney na Melbourne ilishindana juu ya nafasi ya mji mkuu. 1908 azimio la kujenga mji mpya likafanywa mahali kati ya miji miwili mikubwa.

Neno "Canberra" lina asili katika lugha ya [Aborigini|Maaborigini]] walio wenyeji asilia wa Australia. Maana yake ni "mahali pa mkutano".