Namba
Mandhari
(Elekezwa kutoka Nambari)
Namba (au nambari) ni dhana na lugha inayotumiwa kutofautisha idadi au kupima kiwango. Namba zinazojulikana zaidi ni zile namba asilia kama vile 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10 na kadhalika.
Utaalamu unaoshughulika habari za namba ni hasa hisabati pamoja na matumizi yote yake katika fani kama vile uhandisi, uchumi, takwimu na sayansi mbalimbali. Hisabati inatumia dhana ya "namba" kwa upana mkubwa hata nje ya namba asilia. Hisabati inajua
- namba asilia kama 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10.
- Humo tunatofautisha namba kivunge na namba tasa.
- 0 yaani sifuri
- namba hasi -1, -2, -3 ....
- namba kamili (integer) zinazojumlisha namba asilia, sifuri na namba hasi. Namba hizi huandkiwa kirahisi kwa kutumia tarakimu (numerali) yaani alama zinazoweza kuonyesha namba.
- Humo tunatofautisha namba shufwa na namba witiri.
- namba wiano yaani kila namba inayoweza kuandikwa kwa umbo la sehemu kama vile , , , , na kadhalika au pia kuandikwa kwa mfumo desimali kama vile 4, 0.5, 0.04, 2.5 na kadhalika.
- namba zisizowiana zisizolingana na sehemu, kwa mfano namba ya duara π (Pi) ambayo haiwezi kuandikwa kikamilifu kwa kutumia tarakimu.
- namba halisi zinazojumlisha namba kamili, namba wiano na namba zisizowiani, yaani namba zote ambazo zingeweza kutokea katika mstari endelevu.
- namba changamano ambazo zina sehemu mbili, ya kwanza ni namba halisi, na ya pili ni namba inayofikiriwa tu.
- namba tasa zisizogawiwa kwa namba nyingine isipokuwa kwa 1 na kwa namba yenyewe.