Nenda kwa yaliyomo

Usawa (hisabati)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Namba witiri)

Usawa (kwa Kiingereza parity) katika hisabati unamaanisha ya kwamba kila namba kamili (integer) iko katika moja ya makundi mawili: namba shufwa kama 2, 4, 6, 8 au namba witiri kama 1, 3, 5, 7.

Kwa hiyo jumla ya namba kamili hugawiwa katika makundi mawili yenye idadi sawa za namba. Kwa mfano kuanzia moja hadi kumi namba shufwa na witiri zinapokezana na zinaendelea mfululizo vile bila mwisho: 1, 2, 3, 4, 5, 6, 7, 8, 9, 10

Namba huitwa "shufwa" kama inaweza kugawiwa kwa 2 bila kuacha baki. Kama si vile ni namba witiri.

Kwa mfano 6 ni shufwa kwa sababu hakuna baki tukiigawa kwa 2: 6 : 2 = 3, bila baki.

Kinyume chake 3, 5, 7, 21 ni witiri kwa sababu zinaacha baki la 1 baada ya kuzigawa kwa 2.

3:2 = 1, inabaki 1

7:2 = 3, inabaki 1

21:2 = 10, inabaki 1.

Mifano ya namba shufwa ni −4, 0, 8 na 1734. Mifano ya namba witiri ni −5, 3, 9 na 73.

Hisabati kwa namba shufwa na witiri

[hariri | hariri chanzo]

Kujumlisha na kutoa

[hariri | hariri chanzo]

shufwa ± shufwa = shufwa; (4+2=6; 8-4=4)
shufwa ± witiri = witiri; (4+3=7; 8-3=5)<
witiri ± witiri = shufwa (3+5=8; 7-3=4)<;

Kuzidisha

[hariri | hariri chanzo]

shufwa x shufwa = shufwa; (2x4=8)
shufwa x witiri = shufwa; (2x3=6)
witiri x witiri = witiri; (3x5=15)

Kwa ugawaji matokeo ni tofauti kwa sababu kugawa namba kamili kwa namba kamili inaweza kuleta tokeo ambalo si namba kamili, kwa mfano 2:8 = 1/4 ambayo si namba kamili. Namba zisizo kamili si shufwa wala witiri.

Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Usawa (hisabati) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.