Nenda kwa yaliyomo

UNICEF

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Unicef)
Jengo la UNICEF Bangkok

UNICEF (United Nations Children's Fund) au Mfuko wa Kimataifa wa Watoto ni shirika la Umoja wa Mataifa kwa shabaha ya kuwasaidia watoto duniani. Ina nchi wanachama zaidi ya 160.

Makao makuu yapo mjini New York (Marekani). Shirika liliundwa mwaka 1946 likiitwa "United Nations International Children's Emergency Fund" kwa nia ya kuwasiadia watoto wa Ulaya waliokumbwa na njaa na magonjwa katika zilizoharibiwa katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Leo inashughulika miradi ya kupambana na maradhi miongoni mwa watoto, kuboresha elimu na haki za watoto.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: