Chuo Kikuu cha Dodoma
Chuo Kikuu cha Dodoma | |
---|---|
University of Dodoma | |
Wito | Embracing Knowledge |
Staff | 950 |
Wanafunzi | 26000 |
Mahali | Dodoma, Tanzania |
Tovuti | https://www.udom.ac.tz/home |
Chuo Kikuu cha Dodoma (kifupisho chake ni UDOM) ni chuo kikuu ambacho bado kinajengwa mjini Dodoma, Tanzania. Ujenzi unafanyika katika kipande cha ardhi cha hekta 6,000 karibu na Dodoma, kilomita 400 magharibi kutoka jiji la Dar es Salaam na kilomita 7 kutoka Dodoma mjini.
Mafunzo yalianza rasmi septemba mwaka 2007, wakati wanafunzi zaidi , walijiunga na programu zilizotolewa katika vitivo vya Humanities, Sayansi ya Ujamaa, Elimu na 'Informatics and Virtual Education'(Elimu angavu). Vyuo vya Sayansi ya Maisha na Afya na Sayansi zinazolingana zilianzishwa mwaka.Hivi sasa UDOM ndicho chuo kikuu kinachokuwa kwa kasi nchini, ni kikubwa kuliko chuo kikuu chochote ndani ya nchi, na kinasifiwa kwa kutoa watahiniwa wenye uwezo na uwezo wa kushindana katika soko la ajira.
Sambamba na Maono ya Nchi ya Maendeleo ya 2025, Chuo Kikuu cha Dodoma, kikishamalizika kamili, kitaweza kuwachukua wanafunzi 40,000 katika taaluma mbalimbali. Hii ni zaidi ya mara mbili ya ukubwa wa sasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Hata hivyo, chuo kikuu cha Dodoma bado kipo katika maendeleo. [1]
Kilitangazwa kuwa chuo namba mbili (2) kwa ubora wa elimu nchini Tanzania mnamo Machi 2018, kikitanguliwa tu na chuo kikuu cha Dar es Salaam.Mpaka mwwaka 2018 chuo kikuu cha Dodoma kilikuwa na vitivo saba, vikiwa na insia zenye kozi tofautitofauti.
Chuo kikuu cha Dodoma kwa sasa kina ndaki saba: Ndaki ya Sayansi ya Ardhi, Ndaki ya Sayansi Asilia na Hisabati, Ndaki ya Informatics na Virtual Education(Elimu angavu), Ndaki ya Elimu, Ndaki ya Binadamu na Sayansi ya Jamii, Ndaki ya Afya na Sayansi Shirikishi na Ndaki ya Mafunzo ya Biashara na Sheria, hivi karibuni pia kumeanzishwa ndaki mpya za kitaaluma ndani ya Ndaki ya Binadamu na Sayansi ya Jamii UDOM kilichopewa jina la Taasisi ya Masomo ya Maendeleo (IDS) chenye jukumu la kuimarisha wataalamu ndani ya fani ya Masomo ya Maendeleo.
Chuo hiki kikuu hutoa programu mbali mbali za shahada ya kwanza na wahitimu kutoka karibu nyanja zote za maarifa.
Katika Ndaki ya elimu, programu kadhaa za shahada ya kwanza hutolewa kwa kuzingatia masuala yanayoikabili sekta ya elimu nchini Tanzania na nje ya nchi. Kuna digrii 11 tofauti za bachela katika chuo cha elimu.
Ndaki ya Elimu angavu (Informatics and Virtual Education) inajulikana sana kwa umahiri wake katika fani ya Tehama nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla.Ndaki hii inatoa programu za shahada ya kwanza na uzamili katika maeneo kama vile sayansi ya kompyuta, uhandisi wa kompyuta, uhandisi wa mawasiliano ya simu, usalama wa habari, mifumo ya taarifa za afya na biashara na programu nyinginezo nyingi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi Archived 9 Machi 2010 at the Wayback Machine.
- Chuo Kikuu cha Afrika Kusini Archived 28 Julai 2011 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Dodoma kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |