Nenda kwa yaliyomo

Dodoma (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wilaya ya Dodoma mjini)


Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma is located in Tanzania
Jiji la Dodoma
Jiji la Dodoma
Majiranukta: 6°10′23″S 35°44′31″E / 6.17306°S 35.74194°E / -6.17306; 35.74194
Nchi Tanzania
Mkoa Mkoa wa Dodoma
Halmashauri Halmashauri ya jiji la Dodoma
Kata 41
Mitaa 222
Serikali[1]
 - Aina ya serikali Halmashauri ya jiji
 - Mstahiki Meya Davis G. Mwamfupe
 - Mkurugenzi wa Jiji Joseph C. Mafuru
Idadi ya wakazi (2022)https://www.nbs.go.tz
 - Wakazi kwa ujumla 765,179
EAT (UTC+3)
Msimbo wa posta 411xx
Kodi ya simu 026
Tovuti:  Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Mkuwa wa Dodoma

Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania na pia ni Jiji.

Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973, lakini mnamo tarehe 26 Aprili 2018 katika maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano John Magufuli aliupandisha hadhi na kutangaza rasmi kuwa Dodoma ni Jiji.[2][3] [4][5][6] Ofisi kuu za wizara na taasisi nyingi za serikali hatimaye zilihamia Dodoma katika miaka 2016 - 2019.[7][8]

Jiji hili pia ni makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na eneo lake linahesabiwa kama Wilaya ya Dodoma yenye postikodi namba 41100[9].

Eneo la mji liko mita 1135 juu ya usawa wa bahari UB. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji wa Dodoma ulikuwa na wakazi wapatao 410,956 waishio humo.[10]: 17  Mwaka 2022 walihesabiwa 765,179 [11].

Asili ya jina

[hariri | hariri chanzo]

Neno "Dodoma" linasemekana kumetokana na neno la Kigogo "dodomia" kufuatilia historia kwamba zamani kuna tembo alikuja pale mjini akakita nyayo zake ardhini akiacha alama ya nyayo zake zimedidimia.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Dodoma ilianzishwa mwaka 1910[12] wakati wa ukoloni wa Kijerumani kama kituo kwenye reli ya kati penye karahana ya reli. Tangu mwaka 1912 imekuwa makao makuu ya Mkoa wa Dodoma wa D.O.A..

Mwaka 1913 Dodoma ilikuwa na posta, simu, hoteli na maduka 26 (moja ya Mzungu, mengine ya Wahindi na Waarabu). Kikosi cha polisi kilikuwa na askari 59.

Dodoma imeendelea kuwa mji mdogo mpaka kutangazwa kuwa mji mkuu. Azimio hili lilileta ujenzi wa maofisi kadhaa ya serikali.

Kwa ujumla uhamisho ulichelewa kwa sababu mbalimbali; sababu muhimu ni ya kwamba watumishi wa serikali na wanasiasa walio wengi hawakupenda kuondoka katika jiji halisi na kuhamia mji ambao ni mbali sana na mazingira waliyoyazoea. Pia matatizo ya kifedha yalisaidia kutangaza nia ya kuhamia lakini kubaki palepale.

Hali halisi bunge lilikuwa linakutana Dodoma lakini makao ya kikazi ya serikali ya Tanzania yalibaki Dar Es Salaam pamoja na ikulu ya rais hadi mwaka 2016. Ndipo kwa amri ya rais mpya, John Magufuli, sehemu kubwa ya ofisi za wizara zimepelekwa Dodoma. Ofisi nyingi zimejengwa katika kata ya Mtumba, takriban kilomita 30 utoka kitovu cha jiji[13].

Kiuchumi ni kitovu cha kilimo na biashara ya karanga, maharagwe, alizeti na mizabibu, pamoja na mifugo na kuku. Pia Dodoma ni mji unaosifika kwa ulimaji wa zabibu na uvunaji wa ubuyu.

Elimu inahitaji kuboreshwa, hasa maeneo ya vijijini, maana ndio mji mkuu: hivyo kunahitajika kuboreshwe zaidi.

Mawasiliano

[hariri | hariri chanzo]

Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Dar Es Salaam, pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo na barabara ya kale ya "Cape Town - Cairo" inayopitia Dodoma kutoka kaskazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini (Iringa). Barabara nyingine ni za udongo tu.

Kuna pia njia ya reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara.

Dodoma ina uwanja wa ndege wa kitaifa na vyuo vikuu, kikiwemo kile kikubwa zaidi Afrika Mashariki.

Dodoma kuna makao makuu ya Kanisa la Biblia Publishers pamoja na Emmaus Shule ya Biblia.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Halmashauri ya Jiji la Dodoma". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Juni 2022. {{cite web}}: |archive-date= / |archive-url= timestamp mismatch; 19 Juni 2022 suggested (help)
  2. https://www.ikulu.go.tz/index.php/media/press_release# Archived 2 Machi 2018 at the Wayback Machine. tovuti ya ikulu iliangaliwa tar 26 April 2018
  3. https://globalpublishers.co.tz/rais-magufuli-atangaza-dodoma-kuwa-jiji-video iliangaliwa 26 Aprili 2018
  4. https://www.youtube.com/watch?v=FPqrlspV0zI iliangaliwa 26 Aprili 2018
  5. https://www.youtube.com/watch?v=TWdZAa_-syQ iliangaliwa 26 Aprili 2018
  6. https://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/24212-dodoma-yasubiri-baraka-kuwa-jiji Archived 26 Aprili 2018 at the Wayback Machine. iliangaliwa 26 Aprili 2018
  7. http://www.mwananchi.co.tz/habari/Serikali-kuhamia-Dodoma/1597578-3295558-wvnu7h/index.html
  8. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-26. Iliwekwa mnamo 2018-04-26.
  9. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-07.
  10. "Ripoti ya Sensa 2012" (PDF) (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 2022-03-26. Iliwekwa mnamo 2022-07-03.
  11. https://www.nbs.go.tz
  12. Deutsches Kolonial-Lexikon (1920), vol I, uk. 529 ff., makala "Eisenbahnen" ( I. Deutsch-Ostafrika, b) Mittellandbahn)(online hapa Archived 10 Juni 2021 at the Wayback Machine.)
  13. President Magufuli: I’ve finally moved to Dodoma; Citizen 13.10.2019, lookup Juni 2022
Kata za Wilaya ya Dodoma mjini - Mkoa wa Dodoma - Tanzania

Chahwa | Chamwino | Chang'ombe | Chigongwe | Chihanga | Dodoma Makulu | Hazina | Hombolo Bwawani | Hombolo Makulu | Ihumwa | Ipagala | Ipala | Iyumbu | Kikombo | Kikuyu Kaskazini | Kikuyu Kusini | Kilimani | Kiwanja cha Ndege | Kizota | Madukani | Majengo | Makole | Makutupora | Matumbulu | Mbabala | Mbalawala | Miyuji | Mkonze | Mnadani | Mpunguzi | Msalato | Mtumba | Nala | Nghong'onha | Nkuhungu | Ntyuka | Nzuguni | Tambukareli | Uhuru | Viwandani | Zuzu