Zuzu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Zuzu ni kata ya Dodoma Mjini katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6485 [1] waishio humo.

Kata ya Zuzu ina jumla ya mitaa 5 ambayo ni Mtaa wa Mazengo, Mtaa wa Pinda, Mtaa wa Sokoine, Mtaa wa Chididimo na Mtaa wa Soweto.

Wakazi wa kata hii ni hasa wakulima na wafugaji pia ni wafanyabiashara.

Kata ina jumla ya shule 3 za msingi ambazo ni S/m Zuzu, S/m Chididimo na S/m Soweto ambayo ni mpya kwa sasa.

Pia kata ina shule moja ya sekondari ambayo ni Shule ya Sekondari Zuzu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Dodoma - Dodoma MC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
Kata za Wilaya ya Dodoma mjini - Mkoa wa Dodoma - Tanzania

Chahwa | Chamwino | Chang'ombe | Chigongwe | Chihanga | Dodoma Makulu | Hazina | | Hombolo Bwawani | Hombolo Makulu | Ihumwa | Ipagala | Ipala | Iyumbu | Kikombo | Kikuyu Kaskazini | Kikuyu Kusini | Kilimani | Kiwanja cha Ndege | Kizota | Madukani | Majengo | Makole | Makutupora | Matumbulu | Mbabala | Mbalawala | Miyuji | Mkonze | Mnadani | Mpunguzi | Msalato | Mtumba | Nala | Ng'hong'honha | Nkuhungu | Ntyuka | Nzuguni | Tambukareli | Uhuru | Viwandani | Zuzu