Mkoa wa Dodoma (DOA)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maeneo ya Mkoa wa Dodoma wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Mkoa wa Dodoma ulikuwa mmojawapo kati ya mikoa 21 ya koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (D.O.A., Deutsch Ostafrika) iliyokuwa mtangulizi wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi wa leo.

Mkoa huu ulikuwa na eneo la kilomita za mraba 70,700. Ulianzishwa baada ya kujengwa kwa reli ya kati kwa kuunganisha sehemu za mikoa ya awali ya Mpwapwa na Kilimatinde.

Makao makuu (kwa Kijerumani Bezirksamt) yalikuwepo Dodoma iliyoanzishwa mwaka 1910 kama kituo cha karakana kwenye reli iliyoanza kusafirisha abiria hadi hapo tangu 1 Novemba 1910. Ofisi ndogo ya mkoa (Bezirksnebenstelle) ilikuwepo Mpwapwa. Kombania ya 4 ya Jeshi la Ulinzi wa Koloni ilikaa Kilimatinde, kikosi kidogo Singida.

Mkoa huu ulipakana na

Mwaka 1913 kulikuwa na wakazi Waafrika 299,400 pamoja na Wazungu 117.

Takwimu ya Wajerumani ilihesabu walowezi Wazungu 5 waliofuga ng'ombe 875, kondoo au mbuzi 248, nguruwe 1305 na punda 67. Kwa jumla km² 106 zilitawaliwa na walowezi wa makampuni ya Wazungu. Wenyeji Waafrika walikuwa na ng'ombe 392,250 kondoo na mbuzi 318,660 na punda 6,000.

Kabla ya 1914 yalikuwepo makampuni ya biashara ya kizungu 3 nje ya walowezi 9, halafu maduka au nakanuni 45 ya Wahindi na Waarabu.