Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Bismarckburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mkoa wa Bismarckburg (DOA))
Ramani ya Mkoa wa Bismarckburg (Kasanga) DOA.

Mkoa wa Bismarckburg ulikuwa mkoa mmojawapo kati ya mikoa 21 ya koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (DOA, Deutsch Ostafrika) iliyokuwa mtangulizi wa nchi za Tanzania (bara), Rwanda na Burundi za leo. Makao makuu yalikuwa Bismarckburg, Kasanga (Ufipa) ya leo.

Maeneo yake yalikuwa sehemu ya Mkoa wa Ujiji na kuwa mkoa wa kujitegemea tangu mwaka 1913.

Eneo na mipaka

[hariri | hariri chanzo]

Mkoa huo ulikuwa na eneo la kilomita za mraba 90,400. Eneo hilo lililingana na Mikoa ya Rukwa na Katavi pamoja na sehemu za Kigoma na Tabora ya leo. Bismarckburg ilikuwa mkoa wa kawaida tangu mwaka 1913, ilianzishwa kama mkoa wa kijeshi chini ya utawala wa afisa mkuu wa jeshi la Schutztruppe katika eneo hilo.

Makao makuu (kwa Kijerumani: Bezirksamt) yalikuwepo kiasili pale Bismarckburg (leo Kasanga) kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Mkoa huu ulipakana na

Mwaka 1913 kulikuwa na wakazi Waafrika 81,700 pamoja na Wazungu 76 na Wahindi au Waarabu 47.

Takwimu ya 1913 haikutaja idadi ya walowezi Wazungu waliofuga jumla ya ng'ombe 810, kondoo au mbuzi 431 na nguruwe 157. Waafrika walikuwa na ng'ombe 2,180, kondoo 22,680 na mbuzi 14,200

Mjini Bismarckburg kulikuwa na maduka 5 ya Wahindi. Mji uliunganishwa na waya ya telegrafu Ujiji - Cape Town (Afrika Kusini), iliyoruhusu mawasiliano pia na Dar es Salaam kupitia Afrika Kusini na Zanzibar.