Hifadhi ya Tarangire

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ina ukubwa wa kilometa za mraba 2850 na iko umbali wa kilometa 118 Kusini Magharibi mwa mji wa Arusha nchini Tanzania.

Hifadhi hii ni maarufu kwa makundi makubwa ya tembo kuliko hifadhi nyingine nchini Tanzania. Unaweza kuona kundi la tembo zaidi ya mia tano kwa mara moja.

Makundi ya tembo ndani ya hifadhi ya Tarangire

Hifadhi hii pia ina mandhari nzuri ya kuvutia inayotokana na maumbile ya mibuyu inayosadikiwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka elfu nane.

Wanyama wa aina nyingi wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na punda milia, nyumbu, swala, simba, nyati, kongoni, chui, duma na wengine wengi pamoja na aina 550 za ndege .

Hifadhi hii ni maarufu katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania kutokana na wageni wengi, kutoka ndani na nje ya nchi kwani hupenda kutembelea hifadhi hii. Umaarufu mwingine wa hifadhi hii ni pamoja ya aina ya chatu walio na uwezo wa kukwea miti.

Pundamilia ndani ya hifadhi ya Tarangire

Kutokana na umaarufu huu idadi ya wageni wanaotembelea hifadhi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Unaweza kutembelea hifadhi hii wakati wote wa mwaka na kuwaona wanyama wote bila matatizo kutokana na mazingira mazuri ya hifadhi yanayosaidiwa na Mto Tarangire unaokatiza katikati ya hifadhi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]