Fonimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Fonimu ni jina linalotumiwa katika elimu ya fonolojia kwa kutaja sauti za lugha fulani zilizo sehemu ndogo kabisa za maneno na kuunda tofauti za kimaana kati ya neno moja na lingine.[1]

Katika lugha ya Kiswahili tunaweza kutofautisha fonimu za aina tatu:

  • Fonimu za irabu ambazo ni a - e - i - o - u
  • Fonimu za nusu irabu ambazo ni w - y
  • Fonimu za konsonanti ambazo zinaonyeshwa kwa herufi za b - ch - d - f - g - h - j- k- l - m - n - p - r - s - t - v - w - z; pamoja na hayo kuna fonimu zaidi zinazoonyeshwa kwa kuunganisha herufi mbili kama vile dh - th - ng - ng`- kh.

Wataalamu wanatofautiana juu ya namba ya fonimu za Kiswahili kama ni kwa jumla 33 au 37. [2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Concise Oxford English dictionary
  2. Susan Choge, Understanding Kiswahili Vowels, in The Journal of Pan African Studies, vol.2, no.8, Machi 2009, pp 62-77
Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fonimu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.