Tunduma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kata ya Tunduma
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Tunduma
Idadi ya wakazi
 - 97,562

Tunduma ni mji wa Tanzania kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia. Kuna vituo vya mpakani kwa ajili ya usafiri kwenye barabara kuu ya TANZAM na reli ya TAZARA. Mji unaendelea upande wa Zambia kwa jina hilihili.

Upande wa Tanzania Tunduma imekuwa halmashauri yake katika mkoa wa Mbeya, hadi 2012 ilikuwa kata ya Wilaya ya Mbozi. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji ulikuwa na wakazi wapatao 97,562 waishio humo. [1]

Msimbo wa posta ni 53901 .

Pamoja na kuwa kituo cha mpakani ni pia njiapanda muhimu kwa sababu njia za kwenda Sumbawanga na Ileje zinaachana hapa na barabara kuu ya TANZAM.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 2012 Population and Housing Census General Report (en). Government of Tanzania. Iliwekwa mnamo 2013-11-21.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Tunduma - Mkoa wa Mbeya - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Tunduma


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tunduma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.