Wilaya ya Busekelo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wilaya ya Busekelo ni kati ya wilaya mpya nchini Tanzania zilizoanzishwa kuanzia mwaka 2013. Wilaya hii ilimegwa kutoka kwa Wilaya ya Rungwe ikiwa ni wilaya ya Mkoa wa Mbeya.

Wilaya inapakana na Wilaya ya Kyela upande wa kusini, Wilaya ya Rungwe upande wa magharibi, Wilaya ya Makete upande wa mashariki na Wilaya ya Mbeya Vijijini upande wa kaskazini. Makao makuu yapo Lwangwa takriban kilomita 47 kutoka Tukuyu.

Eneo la wilaya ni km² 969.14 na asilimia 85 zina matumizi ya kilimo, asilimia 15 ni misitu na milima ambayo ni hasa volkeno ya Mlima Rungwe na Milima ya Livingstone. Wilaya inapokea wastani ya milimita 900 za mvua kwenye nyanda za chini na hadi milimita 2700 kwenye nyanda za juu. Halijoto ni ya wastani kati ya sentigredi 18° – 25°.

Hadi 2016 kulikuwa na tarafa moja ya Busekelo na kata 11 pamoja na vijiji 56. Idadi ya wakazi wakati wa sensa ya 2012 ilikuwa watu 96,348 katika kaya 2,773.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Busekelo - Mkoa wa Mbeya - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Isange | Itete | Kabula | Kambasegela | Kandete | Kisegese | Lufilyo | Lupata | Luteba | Lwangwa | Mpata | Mpombo | Ntaba