Milima ya Kipengere

Majiranukta: 9°30′S 34°10′E / 9.500°S 34.167°E / -9.500; 34.167
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Milima Livingstone)
Mandhari ya milima ya Kipengere na misitu yake.

Milima ya Kipengere (kwa Kiingereza: "Kipengere Range" au "Livingstone Mountains") iko kusini magharibi mwa Tanzania kwenye ncha ya kaskazini ya Ziwa Malawi.

Milima yake ya kaskazini inaitwa pia Milima ya Poroto na ile karibu na ziwa inaitwa pia Milima ya Ukinga.

Ni safu ya milima inayoelekea kusini mashariki kutoka bonde la mto Ruaha Mkuu upande wa kaskazini hadi lile la mto Ruhuhu upande wa kusini kwa kufuata Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Kilele chake ni Mlima Jamimbi (mita 2,400 juu ya usawa wa bahari) unayoshuka moja kwa moja ziwani.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]


9°30′S 34°10′E / 9.500°S 34.167°E / -9.500; 34.167