Wilaya ya Makete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mahali pa Makete (kijani) katika mkoa wa Iringa katika ya umegaji.

Wilaya ya Makete ni wilaya moja ya Mkoa wa Njombe. Makao makuu ni Makete mjini (Iwawa).

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 106,061 [1].

Hata hivyo idadi hiyo inawezekana kupungua zaidi siku za usoni, kutokana na idadi kubwa ya watu wake kukimbilia mijini: hiyo ni kwa sababu ya uchache wa huduma za jamii, kama vile shule, hospitali, mawasiliano, pamoja na mfumuko wa bei n.k.

Sababu nyingine ni uenezi wa UKIMWI katika wilaya hiyo ambayo inashika nafasi ya kwanza kwa maambukizi nchini Tanzania.

Wenyeji wa Makete ni Wakinga wanaotumia lugha iitwayo Kikinga.

Aidha yapo makabila mengine kama Wawanji wanaoishi maeneo ya bonde la Matamba ambapo tarafa za Matamba na Ikuwo hasa ndiko kabila la Wawanji wanakoishi.

Tokea miaka ya 2000 kabila hili lilianza kufahamika sana nchini Tanzania kutokana na watu wake kuenea maeneo mengi wakijishughulisha na biashara mbalimbali, hususani biashara ya maduka ambayo imepelekea kuwapatia umaarufu mkubwa katika fani hiyo.

Maeneo ambayo watu hao wameenea kwa wingi ni kama vile Mbeya, hususani wilaya ya Tunduma, Dar es Salaam (Kariakoo) na Songea.

Chakula maarufu katika wilaya hii ni viazi ambavyo pia hutengenezwa ugali uitwao usuge ambao ni mchanganyiko wa viazi na unga au maharage.

Kilimo cha biashara ni pareto na miti ya mbao na matunda.

Wilaya hii pia inasifika kwa kilimo cha ngano na mahindi.

Hali ya hewa Makete ni baridi kiasi kwa maeneo ya kata kama za Kitulo, Mang`oto, Iwawa, Ipelele, Iniho, lakini maeneo mengine huwa na joto kiasi.

Katika siasa wilaya hii imeongozwa na wabunge watatu toka ianzishwe nao ni Tutemeke Sanga, ambaye ni marehemu kwa sasa, Hansi Kitine na Binirithi Mahenge ambaye yupo mpaka sasa anaongoza.

Utamaduni wa wilaya hii ni ngoma ya asili iitwayo Kivilela ambayo huchezwa na wanaume wakiwa na njuga na wanawake pia.

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Makete - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bulongwa | Ikuwo | Iniho | Ipelele | Ipepo | Isapulano | Itundu | Iwawa | Kigala | Kigulu | Kipagilo | Kitulo | Lupalilo | Lupila | Luwumbu | Mang'oto | Matamba | Mbalatse | Mfumbi | Mlondwe | Tandala | Ukwama


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Makete kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.